Utapeli Benki ya CRDB!


Acheni hizo, jaribu kufanya research mjue hapo mwanzo wakati ATM zinaingia mambo yalikuwaje?????????

Sometimes kinachotokea kwetu na huko mnakotaka tufanane nako inategemea na level ya competition na kama hao jamaa wameisharudisha garama zao za KUSIMIKA hizo ATM, THERE MUST BE some reasons!!!!!!!
 

Naona unaongea meeeeengi kujifariji lakini huwezi kubadili ukweli kuwa nilikuwa nikiweka na kuchukua pesa yangu bila kulipishwa chochote..Sasa hiyo habari ya benki kufanyia biashara pesa yangu hilo ni mipango yao, cha msingi nikihitaji pesa yangu naichukua bila makato wala kulipishwa makato ya dizaini ya 'shamba la bibi'. Kwa kifupi huo ndo msingi wa mleta mada, kwamba iweje ulipishwe unapoenda kuchukua chako?

Hayo mengine uliyoandika ni yako mazee na ni njia tu ya kujifariji, lakini nadhani jibu langu umelipata sawa bin sawia.
 

Pundamilia!

Nakushukuru sana kwa jithada zako za kuelimisha hawa akina Tiba na wengine wengi bila kumsahau Abdulhalim! Ukweli ambao hauna mjadala ni kwamba hakuna kitu cha bure hapa duniani labda huko kunakosadikika.

Upeo wa wengi kuliona hilo ni mdogo!!Yes they said and I repeat bure is the most expensive part of all the transactions. Tujifunze kukataa vitu vya bure kwani what we call the hidden cost kwenye vitu wanavyotoa free is quite big. Hata hiyo misaada tunayopewa simply because we are damnly stupid ina hidden cost ambayo ukitafakari ni kubwa kupita kiasi!! Ni heri kufa kuliko kukimbilia hivyo vimisaada uchwara!!

Kwa mfano yule muaji El-Bashir wa Sudan wanaomkingia kifua akina Kikwete na Gadafi huwa haendi kutembeza bakuli EUROPE na USA kama JMK of cause anayo mafuta ya kumtosha na hatapeliwi kama JMK anavyofanywa kwenye madini!! yes !!Angalau ana uwezo wa ku exercise some sort of uhuru wake! Akikanyaga Europe atanyea ndoo !!

Coming back to the subject hata huko ulaya anakorefer mjamaa mmoja people are bitterly complaining on costs for operating ATM and last year ilikuwa ni hot subject kule UK sijui walifikia mwafaka gani but as usual BANKERS know better jinsi ya kuchezea watu shere!! Kama hamtaki kumsikia asemayo Pundamilia mtabakia na ujunga wenu as usual!!!
 
Na mtaongea mengi sana na kujifariji..ila msg sent.
 
Nina Tanzanite account na hawa CRDB... wanasema interest rate ya Tanzanite account ni 0.5 per cent above normal serving rate... nilipowauliza mara zaidi ya 4 ni nini interest rate ya normal serving account mpaka sasa hakuna anayejua...

Nimewauliza mara zaidi ya 6 kuhusiana na tarehe ambapo wanalipa interest rate kwenye hizo account wakasema end of financial year... Nilipowauliza hiyo financial year ya abank inaanza na kuishia lini hakuna anayejua...

Charges kwa kwa kweli ni kubwa maana kwangu mimi wananikata pound sterling 2 (£2) kwa mwezi kwa kutumia internet banking... sijui nini wanacholipia kila mwezi kwenye account yangu ili hali kila ninapojaribu ku-access account yangu servers zao ziko down au unapewa error 404 file not available...
Sisemim kwamba ni wezi maana tumefungua account kwa hiari yetu tukijua kwamba kuna baadhi ya makato...Ninachowalalamikia ni kuwa wako so deceptive kiasi kwamba charges zao haziko wazi... walisha wahi kuniambia kwamba kama account yako haijatumika kwa muda basi ili uiondoke kwenye u-domant inabidi uwalipe £5 sterling...

Nangojea tu nirudi Bongo ili nikakimbe kilicho changu na kufunga a/c yangu maana hawa Crdb hawajui namna ya kumjali mteja... Mteja kwao ni njoe ufungue a/c ili wafaidike na makato bila kutoa huduma nzuri...
 
Last edited:

Mkuu Pundamilia,

Tuko pamoja katika hili. Maelezo yako hapo ni sahihi na ndivyo benki zinavyo fanya kazi na kutengeneza faida. Kinachogomba hapa kutokana na mleta mada ni hizi charges ambazo zinaonekana moja kwa moja kwenye statement zikiwa na majina tofauti!!!! lakini kwa huduma ile ile??????

Tiba.
 
I terminated my loan progress. That manager wanted 10% from any deposited money for nothing.
Kuna taasisi za fedha haziruhusu kabisa upuuzi wa mfanyakazi kumwomba mteja kickback. Sifahamu tabia hii imeigwa kutoka wapi.

Nimewauliza mara zaidi ya 6 kuhusiana na tarehe ambapo wanalipa interest rate kwenye hizo account wakasema end of financial year... Nilipowauliza hiyo financial year ya abank inaanza na kuishia lini hakuna anayejua...
Kwenye acc. ya kawaida hapa bongo, nimeona transaction inayofanana hivi:
30Jun Interest to date xyzC
30Jun Withholding tax xyzD


Hii gharama ya ATM ni vyema sasa ikapunguzwa, ukizingatia misururu kwenye counter imekuwa mirefu sana. Waanze kutoa elimu kwa wafanyakazi wao, hali kadhalika kwa wateja ili kuongeza ufanisi.
 
Hebu tutajie huduma gani za msingi ulizokuwa ukizipata bure?

Kuweka na kuchukua pesa.

Abdulhalim,
Mimi nipo kwenye nchi moja hapa Ulaya. Kama ulivyosema huduma za kuweka na kuchukua pesa kwenye kaunta au ATM za benki yao ni bure ila ukitumia kadi yako ya VISA kununua vitu dukani wanakukata kama T.Shs 400 kila unaponunua.

Nikirudi kwenye pointi ta Pundamilia pia kuna ukweli wake kwani mwisho wa mwaka wanakukata kama T.Shs 50,000 ambazo ni karibu T.Shs 4200 kila mwezi. Kwahiyo ni ujanja tu wa kuendesha biashara kwa haya mabenki.
 

Vyema,mchango wako umeeleweka.

Kitu ambacho ndg Pundamilia anachong'ang'ania ni kuwa kila akaunti lazima ulipie makato duniani kote, kitu ambacho si kweli. Kama ulivyoeleweka hapo juu ni kuwa inategemea na huduma unayoitumia..mimi binafsi nilikuwa nikitumia basic services za kuweka na kutoa fedha free of charge through respective bank's ATMs. Ni free na sikuwahi kulipia hata senti tano! Hata credit card ni free! Utakapo-step-out kwenye services za ziada hapo ndio unalipia.

Sasa jibaba linapokuja hapa na kuanza kung'ang'aniza vioja kuwa hoja huwa sina cha kuwafanya ila kuwaacha wajifariji, wanadhania wanachojua wao ndio exclusive na final, kumbe ni kuji-embarass mbele ya kadamnasi.
 

Mkuu Tiba,
Ahsante sana nimekupata vizuri.

Mimi nindhani njia nzuri ya kumsaidia mleta mada, ninamshauri aende katika tawi lolote la CRDB lililo karibu nae na awasilishe maelezo yake, ninahakika CRDB wataweza kumuelimisha juu ya tatizo lake.

Zaidi ya hapo, katika suala kama hili mleta mada hawezi kupata jibu la moja kwa moja kutoka hapa kwenye forum kwani hata sisi tulioletewa hoja tumeijadili kwa kadri ya maelezo yalivyotolewa tu na hakuna ya ziada.

Mwisho, ninashauri ndugu zangu wengine kuwa tunaposaini makaratasi pale benki au kwingineko, tujifunze kuuliza maswali mengi kadri inavyowezekana na pia kuhakikisha yale maandishi madogo sana tunayasoma pia kwani pale ndipo kwenye catch.
 

Mwalimu anapofundisha kuna baadhi wataelewa na kupata 100% na pia kuna wengine hupata 0% hilo ni jambo la kawaida mkuu.
Somo nimekwishalitoa kwahiyo kama hukuweza kupata 100% mimi sina msaada zaidi ya hapo take your 0% then uangalie wapi umekuwa mgumu wa kuelewa. Probably, check your background, inawezekana labda wewe unajua kila kitu hadi umepitiliza kwa ujuaji wako.
Kwaheri!
 

Wewe bana usinitishe na background sijui nini ni my A$$ wala usitake kwenda huko..

Hoja imekushinda kitambo kwa kulazimisha general statements zako za kijinga kuwa eti kila akaunti lazima ilipiwe..Nimekuonesha kuwa your knowledge is LIMITED ON THIS ISSUE..sasa ninapokwambia kuwa nilikuwa na-run akaunts bila makato ya aina yeyote unanibishia HALAFU UNAJIITA MWALIMU my A$$$! Hivi una uzima ktk AKILI YAKO WEYE?
 
MI NAKUSHAURI TU, NENDA BENKI MOJA INAITWA DIAMOND TRUST BANK, hawa jamaa wana free banking kwenye SAVINGS ACCOUNTS; yaan hawana charges yoyote, isipokuwa account yako ikiwa chini ya minimum balance kwa miezi mitatu ndo wanakukata pesa kidogo. Tena wana VISA DEBIT CARD wanatoa bure (International). Hata akaunti za biashara wako chini mno kwa kiwango cha kufungulia na gharama zingine...yan wako fiti kichizi, nenda ujaribu tu!!!
 
Sijawahi kuona bank inayo charge fee kwenye ATM,I mean kama una accoutn na hiyo bank na uanenda kwenye ATM yao there is no way wakaku-charge any fee,unless otherwise unatumia ATM ya bank ambayo ni tofauti na ile unayo bank wewe.
Kwa mfano right una account na Bank of america na unataka kutoa pesa na upo kwenye ATM za citi group of course citi group wata kucharge ATM fee yao lakini kama una withdraw money within ATM za bank of america na ww ni mteja wa bank of america hakuna fee period.
 

It is not like that hapa Bongoland
 
kwa hiyo wanaringa kwa ajili hamna competition
kwa ulaya(uk)
account za bure
unakuta ni visa current account ya kawaida haina charges zozote na interest yao ukiweka hela ni very minimal, kwa hiyo wewe upati faida yeyote lakini wao wanapata faida kwa hela yako kuwa mule na wao kuikopesha, kwa hiyo wateja wakiwa wengi inamaanisha hela nyingi
account za kulipia
charges £10 kwa mwezi
visa current account inakuwa na cheque book na cheque gurantee, insurance ya simu, travel insurance.RAC breakdown recovery na disount katika sehemu mbalimbali

hizo charges zinazotozwa na benki za bongo sio hela za kuendesha ATM bali ni sehemu ya faida. Bank ukiziachia zitakutoza kila kitu
mfano uk kuna kitu kinaitwa late payment na overdrawn charges (hii ni £25 £35 inategemeana na bank). kuna kesi ipo mahakamani bank zinatakiwa ziwalipe watu pesa zote kwa ajili hizi charges, imegundulika kuwa ni part ya faida
 
Si kwamba unafanya zile transaction free. Hawa wenye mabenki hata huku nje wanatechnique zako kuna wengine wana monthly charges regardless the number of withdrawals made during the period, wengine quarterly, Kwahiyo charges zipo kwasababu zile machine zinahitahi services kwa operations na uwezo uwepo wa kununua nyingine zikichoka na zimake profit pia. Kwahiyo costs haipukiki. Ila kwa bongo ni too much. Nakumbuka kuna wakati machine za NBC zinatoa 5,000 tu na kama unahitaji pesa nyingi max 150, 000, kwahiyo unadraw mara nne na transaction costs nazo zinakuwa mara nne. Honestly huu ni wizi. They should, I think have a certain fixed costs regardless of drawings made. Though this might comprise low salaried/income groups
 

There's a reason to believe that, Mawazo kama haya ndiyo yanatufanya kila siku tuwe nyuma. Nani alikwambia gharama zimerudishwa?, wakati kila siku share zinauzwa watu wanainvest kwenye mabank haya?.

Ukweli ni kwamba ATM karibu zote huku ni bure na hakuna charge hata kidogo na ATM zinazocharge wameandika kuwa kunacharge kabla hata hujaweka kadi yako. Suala la Consumer protection laws in developing countries like Tanzania bado ni hadithi. Lazima umueleze mteja ataingia gharama gani?. Nili-apply credit card nikapewa ilikuja na package ya charges zote nikafanya cost-benefit nikaona haifai kwa style yangu nikaipiga chini na sikuchargiwa hata sent moja. japo waliprint credit card na postal costs.

Tatizo la Tanzania kila kitu ni usanii tu, hakuna cha ziada. Hizo hiden costs ni wizi, wizi. Unaposema hakuna cha bure mimi kumpa mtu hela yangu aifanyie biashara namsaidia yeye au ananisaidia mimi?. mabank ya bongo likija suala la kulipa interest wagumu kweli, ila kukata bank charges wako faster.

Tubadilike kufuata mambo mazuri ya wenzetu haimaanishi kuwa, sisi bado tupo stone age hatuwezi kuwafikia. Mawazo haya mgando tuyaondoe tunaweza kabisa kuyaondoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…