Utapeli gani ulifanyiwa hautosahau?

Utapeli gani ulifanyiwa hautosahau?

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Kuna rafiki yangu alinisumulia kwamba, mwaka 2008 akiwa bado mwanafunzi, alikutana na watu wawili waliomsimamisha njiani, wakamuongelesha awaelekeze njia ya sehemu ipo mbali kidogo na walipokutana.

Basi akaacha mambo yake muhimu, akawapeleka hiyo sehemu mwendo wa kama dakika 20 hivi, anasema hapo hata akili ilikuwa kama inafuata kila anachoambiwa na wale watu mithili ya kondoo aliyefungwa kamba shingoni anapelekwa kuchinjwa na wala habishi.

Wakafika hiyo sehemu, wale watu wakashukuru wamewasaidiwa, ila wakaanza kumuambia jamaa (yule rafiki yangu) kwamba wao ni waaguzi wa tiba asili na wameona kuna mtu amemroga jamaa (yule rafiki yangu).

Wale matapeli wakamwambia jamaa (yule rafiki yangu) kwamba kwa kuwa amewasaidia kuwaelekeza njia, basi watamsaidia bure kutatua tatizo lake.

Kazi ikaanza, yule jamaa akatema nywele kutoka mdomoni, akaambia azichome moto, akazichoma. Wakati wote huo jamaa (yule rafiki yangu) alikuwa anaogopa sana kuona ametema nywele kwani ni mara yake ya kwanza.

Basi baada ya hapo, wakamwambia akapumzike nyumbani, ile anafika tu nyumbani, jamaa (yule rafiki yangu) anajisachi mfukoni simu yake imekuwa sabuni na pesa alizokuwa nazo shilingi 80,000 zimekuwa magazeti.

Jamaa (yule rafiki yangu) anasema alichanganyikiwa sana, alitaka arudi alipowaacha lakini sasa hata sura zao alikuwa amezisahau. Kuja kushtuka, ametapeliwa kweupeee….!
 
Back
Top Bottom