Utapeli katika betri za Panasonic AA (TBS mko wapi?)

Utapeli katika betri za Panasonic AA (TBS mko wapi?)

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Kwa mara kadhaa sasa nimenunua betri za Panasonic AA, zenye nembo ya TBS, lakini zimekuwa zinaacha kufanya kazi ndani ya nusu saa, zingine hata siku mbili hazifiki. Na hii ni kwa matumizi madogo tu ya remote control ya TV na mouse ya computer. Hii siyo sawa kabisa, kwa matumizi haya ya kawaida, hizi betri inatakiwa zidumu kwa miezi kadhaa.

Je, TBS hawalijui hilo? Je inawezekana kuna watu wanacharge betri zilizokwisha na kuziweka kwenye package kama mpya na kuzirudisha madukani?

Nina uhakika na wengine wamekumbana na adha hii ila labda watu wameshaona ni kawaida.
 
Hahahaa umenikumbusha mbali sana. Nakumbuka miaka flani ya nikiwa boarding schoool kulikuwa na redio ya bweni sasa siku moja kulikuwa na mechi ya fainali UEFA umeme hakuna nguzo imeanguka basi watu wakapitisha mchango zikanunuliwa betri mpya sealed, kuwekwa kwenye redio ikaongea kama dk 1 halafu ikaanza kukoroma hahahaa watu walichanganyikiwa. Ikabidi tuende kwa muuzaji kuona shida ya wanafunzi akatoa box 2 bure na katika hizo kuna combination moja tuu ndio ilifanya kazi walau kwa siku mbili. Betri ni fake long time sana. Tbs wamelala
 
Hii kitu inaniuma sana. Nilikuwa natumia rechargeable batteries zimedumu miaka karibu 4. Kuna uwezekano zinaharibu hata vifaa unavyotumia ukiachilia mbali usalama wa kutumia hizi betri zenyewe.
 
Back
Top Bottom