Kwa mara kadhaa sasa nimenunua betri za Panasonic AA, zenye nembo ya TBS, lakini zimekuwa zinaacha kufanya kazi ndani ya nusu saa, zingine hata siku mbili hazifiki. Na hii ni kwa matumizi madogo tu ya remote control ya TV na mouse ya computer. Hii siyo sawa kabisa, kwa matumizi haya ya kawaida, hizi betri inatakiwa zidumu kwa miezi kadhaa.
Je, TBS hawalijui hilo? Je inawezekana kuna watu wanacharge betri zilizokwisha na kuziweka kwenye package kama mpya na kuzirudisha madukani?
Nina uhakika na wengine wamekumbana na adha hii ila labda watu wameshaona ni kawaida.