Utapeli mpya Magufuli Terminal

Navyojua mimi kwenye usafiri wa IT hamnaga mabasi mzee, sema matukio kama haya huja na funzo siku nyingine utakuwa mwalimu.

Kwa mazingira kama hayo yakijirudia hutaweza kutapeliwa tena

Wasikudanganye hakuna mtu ambaye ni mjanja wa kila sector, hawa wanaokuona mshamba kwa kutapeliwa nao wana siri zao vifuani mwao.

Hata hao matapeli wa hapo stand waliojifanya ma chek bob wa town, kuna uwezekano wakipandisha city centre pale K/Koo wanalizwa.
 
Mkuu umetoka mbwinde juz juz nn?mbona huelewek?mara IT mara Magufuli terminal....mbona ni vitu viwil tofauti...toka lini IT zikapatikana magufuli terminal....Tena na ticket ukaenda kukatia kabisa 😂😂😂
Pole! ila hyo ndio daslam,ukikaa vibaya watu wanakula kichwa
 
Wewe tambua tu, stand za mabasi hapa Tanzania ni magenge rasmi ya wezi, vibaka, matapeli, wachuuzi na watu wasiokuwa na kazi rasmi. Ukifika hapo uwe makini na usimwamini yoyote.
Huo ndio ukweli wenyewe, stendi za bongo unatakiwa uingie kwa mawazo ya kila mtu ni muongo na tapeli.
 
Karibu Bongo
 
Watu wa Dar, kila gari la "private" wanaliita IT. Mtu anapanda kwenye kagari ka private kutoka Chalinze kwenda Dar, anasema amepanda gari ya IT.
Hivi pia ni kwa nini hizo IT zinaachiwa na mamlaka husika kubeba abiria?
 
Wewe tambua tu, stand za mabasi hapa Tanzania ni magenge rasmi ya wezi, vibaka, matapeli, wachuuzi na watu wasiokuwa na kazi rasmi. Ukifika hapo uwe makini na usimwamini yoyote.
Kabisaaa yaan
 
IT ndo kitu gani!!??
 
Ungeenda zako kibo ungekua special Hire za kutosha za uhakika.
Samahan mkuu hivi zile special hire maana yake nini naziona tu iLa sielewi.........nijuze unitoe tongotongo
 
Siku zote ukiwapelekea polisi kesi ya kipuuzi, huishia tu kukupuuza na kukupotezea. Wakati mwingine kuwa makini.

Kama unataka kusafiri kwa basi, kakatie tiketi ndani ya stendi kwenye basi husika. Na kama unataka kupanda gari la haraka ikiwemo hiyo IT, kasubirie barabarani.
 
Wewe ni mshamba hapo hauna hoja kabisa walikuona zoba ukaingizwa kingi na kama mjanja huwezi kutoa pesa bila kuona basi na hasa likiwa na abiria
Ukiwa wewe ndio abiria wa kwanza utaona abaria gani?
Karipoti tatizo lifanyiwe kazi.
Wapiga debe pale ni kero mno
 
Samahan mkuu hivi zile special hire maana yake nini naziona tu iLa sielewi.........nijuze unitoe tongotongo
Hayo ni magari yaliyosajiliwa rasmi kwa ajili ya kusafirisha abiria wenye shughuli zao binafsi.

Yaani kama unataka kusafirisha msiba, au kusafirisha kundi la watu fulani kutoka sehemu moja kwenda nyingine, mnakodi kwa makubaliano maalum.
 
Nchi ngumu sana hii, ngumu mno. Huwa naona jinsi wapiga debe wanavyozidi kuwa bugdha na kero kubwa sana kwa abiria hapo Mbezi stand ya daladala.

It's sad kwamba hata serikali sidhani inajua nini ifanye. Kila mtu yupo kwa ajili yake na walio wake.
 
Samahan mkuu hivi zile special hire maana yake nini naziona tu iLa sielewi.........nijuze unitoe tongotongo
Zinabeba waombolezaji, kuwa makini.
Jokes tu Mkuu.
Zinakodiwa kwa shughuli maalumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…