Utapeli online: mitandao yote inawafuga hawa matapeli,kuwakamata ndio rahisi sana

Utapeli online: mitandao yote inawafuga hawa matapeli,kuwakamata ndio rahisi sana

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,395
Reaction score
2,391
Wakati usajili wa vitambulisho vya taifa unakuja tuliambiwa ni mwiba kwa matapeli. Je wameisha? Hapana tena wapo sana tu.

Kuna visa kadhaa vya utapeli nimeshukudia kikiwemo juzi tu,dada katapeliwa mbele yangu.

Inashindikana nini kuwakamata hawa watu?
Nilijaribu kumsaidia yule dada nikapiga simu tigo kuripoti tatizo hilo na ikaonekana kashatoa ile hela.

Nikawaambia kwanini msifunge hiyo laini yake akija kurenew mumkamate? Wakadai sio kazi yao

Kama mtandao ukiamua ni rahisi sana kwanza
1.wanajua pesa imetolewa kwa wakala gani.
2. Mawasiliano ya mtu huyo na namba nyingine
3. Minara ambayo anatumia mara kwa mara.
4. Utambulisho wake upo kule,hata kama line imezimwa, kitambulisho kimesajili line zingine kwanin wasimtrack?

Ni kisa kimoja tu mteja wa voda alifungiwa akaunti yake ya mpesa akashindwa kutoa pesa sababu pesa iliingia kimakosa na kuitoa ile pesa 👏👏👏👏 Vodacom

Tukisema wanafugwa tutakosea?
 
Kwani unapotuma hela si inaonyesha majina ya unayemtumia?
Mbona kama unatetea. Hawa jamaa wa "tuma hela kwenye simu hii, jina litakuja la ....." Hawa wanajulikana na majina wanayotumiwa ni halisi, yamesajiriwa na mitandao hiyo. Tumeisha ripoti na hazifungiwi. Tatizo ni nini?
 
Katika ungese wote wa hii mitandao ..eti ukitumaa helaa kwa mtu akatoa wao hawana cha kukusaidia labda uende polis ndo wakusaidie ... Wengne wana vihuduma uchwara vinaitwa jihudumie cha ajabu kuna mda haifanyi kaz hela hairud ..DUNIA SINIA PAKUA UNACHOWEZA n wizi mtupu
 
Swali linaanzia kwako ,kwanini utume pesa kwa mtu usiemjua ?


Hivi huwa mna akili kweli ?

Kila kitu Hadi kutuma pesa unataka Hadi serikali ikwambie.
 
Mkuu kuna sheria ambazo zinamlinda mtumiaji wa mitandao ya simu. Na ndo maana hata polisi hua ni ngumu kupata print out.

Kikubwa ni elimu kutolewa kwa jamii kuhusiana na mobile money transactions.na sio kuwalaumu mitandao ya simu.
 
Swali linaanzia kwako ,kwanini utume pesa kwa mtu usiemjua ?


Hivi huwa mna akili kweli ?

Kila kitu Hadi kutuma pesa unataka Hadi serikali ikwambie.
Mm sijatapeliwa ila najaribu kutoa au kuungana na alichosema mama Samia.

Yani wew kwa maoni yako inaonekana hata ukipewa kazi ya kuwasaidia watu huwezi,umekaa kiubinafsi sana.
Unaamini mawazo yako yanafanana na ya wengine?
 
Mm sijatapeliwa ila najaribu kutoa au kuungana na alichosema mama Samia.

Yani wew kwa maoni yako inaonekana hata ukipewa kazi ya kuwasaidia watu huwezi,umekaa kiubinafsi sana.
Unaamini mawazo yako yanafanana na ya wengine?
We n mjinga tu. Kwanini utume hela kwa mtu usiemjua.

Idiot
 
Ifikie hatua sasa uwekwe utaratibu

Pesa ikiyotumwa itolewe baada ya robo saa.

Ofcourse si muda mrefu wala haitaleta usumbufu wowote ila itaokoa waliokosea na wanaotapeliwa
 
Huu mfumo ndio maana ulikataliwa mataifa ya Ulaya na America. Sio salama
 
Back
Top Bottom