Utapeli tigopesa sasa unatisha!

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Jamani nina ndg yangu amelizwa laki sita asubuhi ya leo. Mteja kaja na pesa cash awekewe ktk akaunti yake. Akamkabidhi wakala na wakala naye akamrushia electronic money. Alipotaka kufanya transaction ya mteja mwingine (baada ya yule kuondoka) ndipo akagundua zile laki sita alizopewa hazimo ndani ya pochi yake. Kwenda tigo, jamaa alishachukua zile alizoingiziwa kwenye akaunti yake!

Eti imekaaje hii jamani mbona inatisha? mnaofanya biashara hii vipi experience zetu jamani? watu wa tigopesa mnalionaje hili?
 
Huyu jamaa ni mzembe.. maana utafanya vipi transactions haujapewa ela?....Sometimes tusiilahumu kampuni...
 
Huyu jamaa ni mzembe.. maana utafanya vipi transactions haujapewa ela?....Sometimes tusiilahumu kampuni...

Naona hujaelewa mkuu au mi ndo sikueleza vizuri. Yaani jamaa (mteja) kampa wakala hela (hiyo cash laki sita) mkononi, huyo wakala akaiweka kwenye pochi/mkoba. Walipomalizana mteja akaondoka kama kawaida. Baada ya muda kidogo ndipo huyo wakala akagundua hizo laki sita hazimo kwenye mkoba. So ni kama zilikuwa za kiini macho hivi
 

Sasa huu si utapeli wa Tigo pesa bali huyo ndugu yako kapambana tu na mjanja kamuingiza kingi mkuu!hii sio ishu ya kuilaumu Tigo kaka!
 
siku nyingine akifanya biashara ya pesa ajaribu kuwa na safebox eeeh....
 
siku nyingine akifanya biashara ya pesa ajaribu kuwa na safebox eeeh....

Preta unahisi kaibiwa? yeye anaamini jamaa kampa pesa kanyaboya, maana yuko peke yake kwenye kibox chake cha biashara, na hakutoka kwenda mahali, kitendo kimefanyika withini very short time.
 
Sasa huu si utapeli wa Tigo pesa bali huyo ndugu yako kapambana tu na mjanja kamuingiza kingi mkuu!hii sio ishu ya kuilaumu Tigo kaka!

Ndo maana ya kuleta hapa JF mkuu ili kupata ushauri zaidi, mawazo namna ya kuepuka, pia kusikia kama kuna wengine nao walicha-experience kitu kama hiki. Tigo nao wanaweza wakashauri zaidi
 
Ndugu yangu thre is nothiung to do with tigo pesa,hapo ni wao wenyewe mtoa pesa na mpokea pesa
 

kama ni hivo hapa issue sio tigo hapa issue ni CHUMA ULETE
 
Bw mito (Balloteli) hapo kuna shaka nyingi sana hasa kwa huyo Bint Wakala wa tigopesa ni wengi tu tunawaona huku huwa wakilizwa wanakimbilia kuwa wametapeliwa. Nasema uongo kwanini 1. Huyo Msichana anazifahamu No. za huyo mteja kwani haruhusiwi mpaka jina la Mteja litokee ndipo amruhusu 2. Huyo Bint hizo No. anazifahamu za huyo Mteja ni kwamba am-Block na kuwaarifu Tigopesa ambapo hapo alipo wana namba za kituo chake na No. za huyo tapeli. Kwa hiyo hela huyo mwizi hatazitumia mpaka suluhu ipatikane. 3. balloteli km kibanda ni chako toa taarifa POLISI na kuwaarifu tigo huyo jamaa hatamaliza hatua 10 atarudi 4. Huyo mtoto ni tapeli wa kutupwa amejuwa wewe upo mbali sana na IT na hujui nakuhakikishia hakuna hela inayopotea. 5. Mbane huyo wakala akuelezea au mtishie unaenda POLISI atasema tu
 

Nashukuru kwa ushauri wako mkuu Ukwaju, ila nadhani hukusoma vizuri posting yangu. Ila kwa taarifa ni kwamba biashara ni ya wakala mwenyewe, hivyo yeye mwenyewe ni mfanyakazi na mmiliki mwenyewe. Mi nimeileta tu hapa kuomba ushauri
 
Ni mazingaombwe au?
Lakini huwezi kuiamini hiyo kitu hadi ikutokee aisee.
 

Asante mkuu, nadhani heading yangu ina-mislead kidogo. Ila ni kwamba jamaa hapanikani hewani na pesa alitoa fasta baada tu ya kutoka pale kwa wakala
 
Hayo mambo yapo, tena shukuru amechukua hiyo laki6 tu!
Ukichukua pesa ya mtu ambaye ni suspect jifanye umedondosha chini then ikanyage halaf ndy utie kwenye droo.
Sisi wapagani ndy tunafanya hivyo, na inasaidia sana, kama wewe unaimani tofauti endelea na imani yako itakusaidia pia.
NAONGEA KWA EXPERIENCE! KAMA HAUAMINI KAA KIMYA USUBIRI SIKU YAKUKUTE.
 
...Mkuu Amoeba hebu fafanua zaidi hapo ili utusaidie sisi Wapagani wenzako! Unapoikanyaga hela unayodhani ni ya mazingaombwe kutatokea nini kitakachokujulisha kuwa hiyo hela ni ya mazingaombwe na hivyo ukanusurika kuibiwa?
 

Hapo kwa redi umenichekesha Amoeba, unaiona ndogo wakati ndo ulikuwa mtaji aisee......
Hebu tufafanulie hiyo experience mkuu
 

Bongo noma arifu, sasa nitawezaje hata kumhisi ili nifanye uliyoeleza??!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…