Kwakweli nachukia sana matangazo ya kitapeli yanayoendelea kwenye mitandao na haswa mtandao wa Facebook. Wapo wanaojifanya ni waganga wa jadi. Masheikh wa visomo na hutengeneza video za matangazo na kuzilipia Facebook kwa ajili ya KUTAPELI.
Hali hii inapelekea watu kupatwa na msongo mbaya sana wa mawazo, kufungwa, na wengine hata kufikia hatua ya kujiuwa.
Nahisi kama TCRA hawafanyi kazi yao ipasavyo, maana kila leo matapeli wanaongezeka na hatuoni hatua Kali zikichukuliwa kwa wahusika. Nashauri serikali ichukulie tatizo hili kama jambo la dharura.