Utapeli unaofanywa na M-bet kupitia odds; Wamejibu na kusema ni shida ya kimtandao

Utapeli unaofanywa na M-bet kupitia odds; Wamejibu na kusema ni shida ya kimtandao

the ultimatum

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2012
Posts
403
Reaction score
116
Wapendwa nawasalimu,

Naomba awali ya yote nieleweke kuwa sababu ya kuandika uzi huu siyo ya kuharibia kampuni ya M-BET kibiashara bali ni kueleza suala lililotokea kwangu na labda kwa wengine pia ambao ni watumiaji wa michezo ya kubahatisha ya mpira wa miguu kupitia kampuni ya M-BET.

Kitendo cha M-BET kupunguza ODDS za ticket iliyokwishachezwa ni cha kitapeli na hakina tafsiri nyingine. Ukiachilia mbali odds zilizokosea kwa mfano ikiwa Barcelona anacheza na Huesca halafu ukakuta Barcelona amepewa odds 13 na Huesca akapewa odds 1.15 hapo moja kwa moja kunamakosa ya kimaandishi ambayo hutokea kwani uwezo wa Barcelona ni mkubwa mno kimantiki alipaswa apewe odds za Huesca Na kinyume chake. Kwa hiyo hapo ni wazi kabisa odds placing zilikosewa kwa huyu kupewa za mwenzake na kinyume chake.

Lakini kuna swala pia lifahamike Odds zinatabia ya kuongezeka au kupungua kwa kadili muda unavyokwenda na hili huwa halihusishi odds zilizokosewa bali ni utaratibu wa kawaida wa kupungua na kupanda kwa odds kulingana na muda na sababu nyingine za kimichezo. Ifahamike kuwa mabadiliko yanayotokea katika muktadha huu hayazihusu tiketi zilizokwishachezwa.

Inapotokea tiketi imechezwa na ikapunguzwa odds zake baadae au kuongezwa huu ni utapeli wa kimichezo ambao unakatazwa kwamujibu wa sheria za michezo ya kubahatisha.

Ninachokizungumza hapa kimenitokea, mkeka huu nilioweka hapa nimeucheza siku mbili nyuma ulisoma takribani 2,300,000 za kitanzania lakini leo pesa imepungua kufikia 1,700,000 za kitanzania. Huu ni utapeli na haukubaliki. Naomba mamlaka za nchi zichunguze swala hili, haya makampuni yanatupiga sana wakati mwengine, na huwa tunatumia pesa nyingi sana haipendezi tunatumia pesa zetu lakinini tunafanyiwa uhuni. Lakini pia huu ni mtego mwingine wa kukwepa kodi au kulipa kodi pungufu kwa mujibu wa sheria. Kampuni ya M-BET nadhani na makampuni mengine yanatozwa kodi 20% ya tiketi zote zinazoshinda, kwa kupunguza kwa makusudi kiasi cha pesa kwenye tiketi ni kupunguza kodi kampuni iliyopaswa kulipwa kama tiketi ingeshinda.

NB: Team M-BET tuungane pamoja kupinga huu upuuzi

Screenshot_2018-10-10-18-39-20.jpeg


===============================================
Nilizungumza nao kwa simu jana wakaniambia kwenye system yao pesa inaonyesha kama ilivyokuwa ya awali hivyo wamenihakikishia nitalipwa kama ilivyokuwa yaani 2,345,000 badala ya 1,700,000. Niliwakumbusha tu kuhusu mabadiliko ya odds kutozigusa tickets zilizolipwa tayari. Picha hii hapa wamenitumia wao kuonyesha kiasi kinachosoma kwenye system yao
 
Hao ni wez MBET kwanza wanakuwekea timu zenye risk, wanakuwekea option zenye risk,makampuni ya wahindi yapo kitapeli,

Nakushauri bet kwa makampuni ya wazungu wapo vzr sana ,odd za kueleweka, option kama zote,

Tumia 1xbet au galsport bet,

Kifupi mzungu yupo fair anataka WIN WIN SITUATION, hawa wahind,wabongo ukiona wameanzisha makampun ya BETTING jua wamekuja kukunyonya, .
 
M-BET uzuri wao ni mmoja tu haukatwi pesa wakati wa kudeposit hata voda wanaokata unarejeshewa kwenye account 1xbet, sportpesa na bikosports makato yake unanua bando kabisa
 
Pole sana ndugu, mim mambo ya M-bet kwa sasa hivi siyafahamu niliacha kubashiri kupitia M-bet tangu Machi 2017, natumia www.sportpesa.co.tz
 
Kamali bwana...nashukuru kanitoa huko maisha yng yalishaanza kuharibika
 
Nilizungumza nao kwa simu jana wakaniambia kwenye system yao pesa inaonyesha kama ilivyokuwa ya awali hivyo wamenihakikishia nitalipwa kama ilivyokuwa yaani 2,345,000 badala ya 1,700,000. Niliwakumbusha tu kuhusu mabadiliko ya odds kutozigusa tickets zilizolipwa tayari. Picha hii hapa wamenitumia wao kuonyesha kiasi kinachosoma kwenye system yao
IMG-20181010-WA0001.jpeg
 
Nilizungumza nao kwa simu jana wakaniambia kwenye system yao pesa inaonyesha kama ilivyokuwa ya awali hivyo wamenihakikishia nitalipwa kama ilivyokuwa yaani 2,345,000 badala ya 1,700,000. Niliwakumbusha tu kuhusu mabadiliko ya odds kutozigusa tickets zilizolipwa tayari. Picha hii hapa wamenitumia wao kuonyesha kiasi kinachosoma kwenye system yaoView attachment 893971
Awali nilijua labda hiyo pesa ni kabla ya kodi...hata hivyo ni vizuri kufuatilia haya makamampuni yanaiba sana kama sio mfuatiliaji..
 
Huyu Mhindi Nmemmanga 290 toka j'mox mpaka sahizi hajaituma....Na Ukiwapigia Hawapokei...Msaada Jaman Anaejua njia ya Alternative Itakayo nisaidia kuwasiliana nao
 
Back
Top Bottom