Utapeli wa biashara ya kuwekeza unaofanywa na kampuni ya FX Fire iliyopo mkoani Mwanza

Watu hawakomagi jamani😎😎😎
 
"Mang'ombe hayaishi mjini hapa."
Sijui hata inakuaje nafikiria hivi huyo mtu anamshawishije mtu hadi anakubali aisee! Pesa ilivo ngumu hivi mtu aje aniambie nimpe anipe 60% dah inabidi tukae chini week zima akinielezea ataizalishaje with vivid examples.🤔 watu wajue tu hamna shortcuts
 
Uyo sio tapeli mkuu
Naweza kumuita Baharia aliehitimu mafunzo kikamilifu kabisa kila siku tunapiga kelele bongo hii "ukiona unaitwa kwenye fursa basi jua wewe ndo fursa" Ila jitu bado HALISIKII kila siku mada ni zilezile Q-net,Smile we care wanaongelewa wanavyotapeli watu ila Jitu bado HALISIKII amakweli wajinga kila siku wanazaliwa wapya

"WAJINGA NDIO WALI WAO"

5 AGAIN
 
Duh poleni wahanga! Ila jamani bado tu hamshtuki na hizi biashara! Mtu anakuahidi kukupa 60% kwa biashara gani hasa hushtuki mtu kukushikia pesa yako?🤷‍♂️ hizi shortcuts zinatukucost.
Watu wanapenda fedha za chapchap zisizofuata kanuni ya utafutaji kiuhalisia matokeo yake ndio hayo wakati soko la hisa lipo ajabu hawajitokezi kuwekeza...kwahiyo hii itakuwa kama KUKU POA hivyo kama ni kweli wazee wataibuka na kuja na kufanya shughuli za upatu na kutaifisha kisha waliowekezwa wataambulia patupu kwa kuwa hela zao wamekeza kwenye shughuli haramu
 
Hivi hao mnaowaita matapeli na mpaka namba zao za simu mnaziweka humu kwa nini hamuwaripoti mahali husika ama hamtaki kumfaidisha DPP ambae amekuwa ndio mnufaika mkuu wa pesaza wapenda vitonga
Wengi sio matapeli. Sheria ya makampuni inasema ukiwekeza faida mnagawana ila na hasara mnagawa pia. Sasa kama kachoka account mnataka mgawane nini kama sio majivu.
Tatizo watu hawaambiwi kama kuna hasara, na ikitokea hakuna ushahidi kama hasara imetokea. Ndio hapo mambo ya subiri nitawatumia baadae inaanza.
 
Hatua ya kwanza kutapeliwa ni tamaa ya kupenda vitu rahisi(shortcut) pili binadamu tumetofautiana vingi, hasa akili, hivyo mang'ombe wanakamulika vizuri tu maziwa yao kwa kutaka shortcut na kicjwani empty set.
 
Ontario akamatwe afungwe jiwe kubwa sana shingoni atupwe baharini tena kati kati ya bahari...
 
Yani uweke pesa halafu akupe 60% hujiulizi ataizalisha vipi?

Mimi nasisitiza wapumbafu wapigwe maana hakuna namna ya kuwasaidi.
 
Yeah.... though bado sio jambo la kukubalika lakn pia shortcuts sio nzuri wabongo tuelewee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…