Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,215
- 3,076
Wadau wenye ufahamu kuhusu hiki kituko kingine CIS, tafadhali mtujuze.
Tunataka tujiridhishe kwanza na maelezo ya kutosha ili tujue umafia unaoendelea.
Twin Towers Billioni 221
CIS Billioni 199
Richmond Billioni 172
Richmond Billioni 23
Meremeta Billioni 155
EPA Billioni 133
Rada Billioni 40
Jumla Billioni 922
Wacha tubaki nyuma kimaendeleo maana mafisadi wamechota zaidi ya Shilingi Trillioni ukiweka na kashfa nyingine za ufisadi bila aibu wala woga!!! 🙁
Twin Towers Billioni 221
CIS Billioni 199
Richmond Billioni 172
Richmond Billioni 23
Meremeta Billioni 155
EPA Billioni 133
Rada Billioni 40
Jumla Billioni 922
Wacha tubaki nyuma kimaendeleo maana mafisadi wamechota zaidi ya Shilingi Trillioni ukiweka na kashfa nyingine za ufisadi bila aibu wala woga!!! 🙁
CIS, hii nilitaka kuigusia siku moja lakini nikasita mtindiowaubongo. Hii mzee mzima Malecela haponi. Hii ndiyo next issue baada ya EPA. Kaaazi kwelikweli
Hapa suluhisho si kuing'oa SISI-M kwani hao watakaoshika wataendeleza wizi kwa kisingizio cha SISI-M.Tuwape hao hao SISI-M ila tuwabane mpaka wazirudishe pesa zote kwani wanawajua.Alafu majority of the money came from Tanzanian taxpayers! Lakini unakuta wananchi tunakaa kimya eti tunasubiri donor countries waje na wao wadai 'good governance' kama kwenye EPA, alafu JK atasema EPA money was not donor money! Alafu eti tutaridhika, oh, it was not donor money but actually our taxpayers money! Safiii!
Dawa hapa ni 2010 kuitoa CCM madarakani, hamna mjadala!
Ahsante Mkuu BAK,...ila naomba uonyeshe kuwa hizo ni USD ($) na si madafu.
Ila katika hili itakuwa vizuri tukipata kidogo jinsi mambo yalivyokuwa na baada ya hapo akina nani walihusika. Magazeti yote toka jana yameficha majina!
Hapa kazi ipo!
Ahsante Mkuu BAK,...ila naomba uonyeshe kuwa hizo ni USD ($) na si madafu.
Ila katika hili itakuwa vizuri tukipata kidogo jinsi mambo yalivyokuwa na baada ya hapo akina nani walihusika. Magazeti yote toka jana yameficha majina!
Baadhi ya kampuni zilizotajwa na wakala huyo wa kukusanya madeni ni pamoja na Kiex Trading Limited inayomilikiwa na Rajab Maranda, anayetuhumiwa kuiba fedha za EPA, Dar es Salaam International School Trust Fund, Andrew Traders, K. Agencies International, Chawe Transport, Simba Resources, Shela Beach Investment na Chichi Interprises.
Hakuna kazi yoyote, usanii mtupu unaendelea. kwa nini huyo Msolopa ameshindwa kuyataja hayo makampuni na kiasi cha fedha kinachodaiwa?
Dark City hizi ni shilingi siyo Dollar kama unataka kwa dollar basi ni sawa na $922 million.
Wana JF,Haya sasa angalieni, hivi kweli tutafika kwa mtaji huu jamani?...jumla ya 180/b zimekopeshwa na hazirudi...Hulka ya maskini kama nilivyosema, huomba kwa mikono miwili akipewa basi sii deni tena.. Atakuwa mkali na matusi makubwa wakati kisha pata..na kesho akianguka nani atakaye kuja kumuinua.. hivi bado somo la maisha yetu sisi wenyewe halijafikia mahala tuka learn kuwa mkopo au msaada ni fadhila ambayo haina kipimo cha malipo..Tunachezea hadi uchumi wa nchi kwa tamaduni za kimaskini jamani...
Ama kweli adui mkubwa wa Umaskini ni umaskini wenyewe!