Utapeli wa ‘hiyo pesa tuma kwenye namba hii’ umeshika kasi, nimegundua mbinu ya kuwazuia, napendekeza haya yafanyike kuwakomesha

Ngoja siku mwanao anaumwa na upo katika harakati za kutuma pesa kwa nurse kama hongo awekewe damu, alafu ghafla unaaambiwa tuma kwenye namba hii, utahisi kabisa nurse anaogopa kukamatwa hivyo anatumia namba ya mtu mwingine, mbonautatuma halafu akili ndio inakuja kukaa sawa baadae..
 
Asipofika polisi ndani ya siku 2 au 3, namba zote zilizosajiliwa kwa NIDA hiyo zinafungwa. Kama yupo hai basi ataenda kwa mtoa huduma wake kuuliza tatizo nini, na hapo ataelekezwa afike polisi.
Cha ajabu ukipiga namba husika unaambiwa haipo au ilifungiwa! Ni wazi mitandao ya simu inahusika isipokiwa inalindwa na TCRA, ni vipi namba isiyokuwepo itumie mtandao husika? TCRA inalo jibu.
 
Hao hao unao washauri nadhani ndio wana wa alert juzi nilitumwa kumtumia mtu hela sasa jana yake baada ya kuongea na huyo mtu nakupewa notification hiyo asubuhi ikaingia mesage mimi nimetumwa unitumie hizo hela kwenye namba hii eh nikashangaa sana .imekuwaje. wakati ni baina yangu mimi na yeye
 
Unataka wanaosababisha matatizo kwa kutofanya mambo rahisi kabisa wafanye mambo magumu ili kuondoa tatizo! Hili haliwezekani. Tatizo la Tanzania kwenye mambo mengi ni kutokuwa na database ya taifa. Nimesema database na siyo vitambulisho. Ukishakuwa na database ya wananchi wote na wageni wote wanaoishi nchini kwako, basi unaweza kafanya mambo mengine mengi bila nguvu nyingi. NB: sikatai kuwa hata sasa hivi kama wangekuwa wawajibikaji, wangeweza kuzuia hizi namba fake kwa urahisi sana. Kosa walilofanya ni kuachia line zisajiliwe mtaani na ''kila mtu''. Usajili wa line ulitakiwa ufanywe na vituo vya polisi tu tena kwa kutumia kanuni maalum ili kuondoa uwezekano wa line fake. Haijalishi hata kama ungetumika muda mrefu kusajili mradi tu matokeo yawe positive.
 
Kwenye hizi kampuni za simu kuna wafanyakazi ambao siyo waaminifu.
 
Nishatuma hz namba Voda hadi nimechoka nao hawajibu tena kama mwanzo.
 
"nullYou have insufficient balance to subscribe the service. But you can dial *137*09*02 to subscribe the service via M-Pesa", huu nao ni utapeli sawa na ule wa tuma kwa namba hii, unatumiwa ujumbe kama vile ulitaka kujiunga wakati hata kitu chenyewe haukijui!
 
Hivi hizi laini feki nyingi kiasi hiki huwa wanazipata wapi? Kwamba zikishafungiwa kesho wanasajili tena kwa NIDA zipi?!
 
Nilivyojibiwa baada ya kuripoti kwa hawa wavietnam 👇





Just imagine hawa wajinga wanavyoentertain utapeli, nimetamani kuwajibu mbovu ni vile tu hiyo sender haina namba
 
Tatizo kubwa ni kuwa, vibaka wanawalenga "wanyongwa" mtaani, sasa unategemea ukienda kumkwapua "mnyongwa" mtaani kwa kidogo alichopata kwa shida nini kitatokea? Walengwa wakubwa wa vibaka ni "wanyongwa" ndio maana mayowe mengi, muende mkawaibie vibopa huko juu muone kama mtaandamwa
 
sijakuelewa mleta mada hasa kwenye point yako ya kwanza, yani unataka kutatua tatizo kwa kuongeza tatizo lingine kubwa zaidi? ivi ni watanzania wangapi wapo huko vijijini au hata mjini ambao ndio wahanga wakubwa wa hawa matapeli wana uwezo wa kuripoti tcra wakipata izi msg? sasa wewe mtu yupo shambani anafanya shughuli zake katumiwa msg ya kitapeli afu ripoti unafunga hapo ndio unatatua tatizo au umeongeza kuna watu mpaka sasa ivi wana simu lkn kuongeza muda wa maongezi lazima aombe msaada kwa mtu sasa uyo ndio umwambie atoe taarifa tcra
 
Elimu itolewe jinsi ya kutuma msg ya namba ya tapeli, ambae hataripoti namba ya tapeli, kifungo au faini itamuhusu, maana unakuwa kama unasupport utapeli..!
 
Huwa najiuliza wanajuaje?

Ukishaongea na mtu kuhusu swala la kutumiana hela tayari unapata sms kwa namba ngeni

Hiyo hela tuma kwa namba hii ile ya zamani imepotea au kasahau namba ya siri

Nina mfano hai wa jamaa yangu alilia kwa utapeli huo😂
 
Airtel wawe makini sana na wafanyakazi wao, ilikuwa tarehe 6 mwezi huu nimetoka tu kuongea na mtu wa airtel kuwa nitamtumia pesa ilikuwa saa 13:08 mchana

Kufika saa 9 mchana nilikuwa bado sijamtumia, kufika saa 15:46 mchana, tapeli anayejiita REHEMA KIBASI akatuma meseji tuma kwenye namba hii.

Ningejichanganya kidogo tu ningemtumia huyo tapeli

Alijuaje nimetoka kuaongea na mtu kuhusu kumtumia pesa? Wenye mitandao tutakuja kuwashtaki kmmmk kuna usenge mwingi unaendelea humo maofisini kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…