Kuna jamaa wamezuka jijini Arusha wakidai wao wanawapa dawa wananchi za kuongeza nguvu za kiume,kutibu kisukari,nk.Jamaa hawa wamediriki kusema eti hata fanta na cocacola haifai kwa matumizi ya binadamu,kwasababu eti ukienda pale Bonite huwezi kukuta magari yameleta machungwa kwa ajili ya kutengenezea fanta orange.Hivi kweli nchi hii serikali itakubali iwanyweshe wananchi wake vinywaji vyenye madhara kwa wananchi wake,serikali iwe macho kwa hawa madokta njaa,mi nawaita njaa sababu wanajiita madokta wakipotosha taaluma kubwa kama hii