Utapeli wa kwenye dawa za nywele

Utapeli wa kwenye dawa za nywele

Me too

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,388
Reaction score
9,333
Habarini wakuu sijui ndio hili jukwaa husika ama laa nyway moja kwa moja husika na heading yangu kiukweli dawa za nywele za sikuizi hazina ubora kabisa naomba mamlaka husika ijaribu kuzichunguza hizi dawa watumiazo wanawake kwaajili ya nyweli.

Yaani unaweka leo dawa alafu unakaa hata wiki mbili hazijakata tayari manywele yameshaotaa na kitana kinakuwa shida kupita kichwani kiukweli zipo tofauti na dawa za miaka ya nyuma ubora umepungua na bei inapanda kwa kasi baadhi ya dawa hizo mnazo tutapeli ili tujikute tunanunua mara 2 kwa mwezi badala ya kukaa hata miezi 3 ndio uset matokeo yake sivo dawa hizo ni

REVLON (kuanzia za box hadi za kawaida)
BEAUTFULL BEGIN (ya sasa) hii huwaga ni ya box tu

Na nyinginezo kiukweli mmenikera sana mnatuzurumu hela zetu huku mnatuuzia dawa hewa ni sawa na ununuapo dawa ya meno alafu ndani wamejaza upepo ukizani dawa ipo nyingi kumbe sivo mnaboa sanaaaaa na hizo bei zenu huku bidhaa haina ubora wala nini mmenikera sana ni bora tu mamlaka husika ifungie hizi dawa kuliko kutunyonya hela zetu alafu dawazenyewe hazina ubora.
 
Haya ni matokeo ya kutokubali ulivyoumbwa.Kwanini usibaki na nywele zako natural ukatia kitu cha mafuta ya nazi??
 
hiz
Na sofn free
Easy wave! Inshort mimi wiki hazifiki zinakuwa zimeshaota! Nliamua kunyoa nikaanza upya kusuka sitaweka dawa tena
o sofln nywele zangu ni ngumu na nnazijua sana huwaga km vile zime expire sijui hazinaga nguvu yaani haya madawa yafungwe kwakweli
bri kubwaaaa kila uchwao alafu ndani hovyo.

ya box 12000 ±±sh unaeka hukai hata wiki 2 kichwa kishajaaq km nungunungu

mxiiiu.
 
Hiyo revlon ndio nilikuwa natumia miaka yote ila nywele zinaota haraka sana.

Nimehamia Movit now, inasemekana angalau hawachakachui
 
inakug
Hiyo revlon ndio nilikuwa natumia miaka yote ila nywele zinaota haraka sana.

Nimehamia Movit now, inasemekana angalau hawachakachui
halimu inabidi uanze kunyoa upya

alafu movit nao si wanavuta wateja soon nao watafanana km VENUS ilivoanzaga na hizo za revlon.

zifungwe tu haya makampuni hayajui kitu.
 
Nyoa kipara kama mimi dada yako uwaachie midawa yao wapake wenyewe
 
Wanaboa sana hasa softn free nywele wik ishaotea
zifungwe tu.

we mwanamke kutwa unashinda saloon mara 2 kwa mwezi inakuja kweli?
wanazani na sisi hatuchoki?

nimewalaani kwakweli.
 
Haya ni matokeo ya kutokubali ulivyoumbwa.Kwanini usibaki na nywele zako natural ukatia kitu cha mafuta ya nazi??
Mbona na wewe hubaki kama ulivyo umbwa? unavaa nguo,kwaniumeumbwa na nguo, unanyoa mavuzi, siuache tu kwani aloyaumba hakujua kuwa yako na kazi yake huko? mnakata kucha za nini basi, ukitaka ubaki kama ulivyo ubwa we utaweza hata kidunchu tu? Mambo ya Mungu tumuachie Mungu.
 
teh teh teh amekuelewa kwakweli.
 
Back
Top Bottom