Utapeli wa Manji katika Soka, anatakiwa atimuliwe na ashitakiwe

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,227
Wadau;

Kuna mambo ambayo ukiya tafakari kwa makini unaona jinsi ambavyo klabu pendwa ya Yanga ambavyo inaongozwa na mwenyekiti tapeli.

Utapeli huu umeenda mbali hadi kujiongezea muda wa kukaa madarakani

Utapeli huu umeenda mbali hadi kutaka kuwabambikizia kesi watu wanaohoji mambo kwenye klabu

Manji amedhihirisha kuwa ni tapeli namba moja baada ya kuwafanya mashabiki na viongozi wote wa Yanga Mandondocha.

Wamewekwa mfukoni na wote wanaitikia NDIO MZEE....

Hata wazee wenye Umri kama wa mzee akilimali wanamwita "Tapeli" huyu Mzee.

Kuonesha Undondocha wa mashabii wa Yanga ..walidanganywa kujengewa uwanja maridadi katikati ya Mto Jangwani unaotiririsha maji yake kwenye bahari ya Hindi.

Mandondocha wa Yanga walitapeliwa wakatapelika...sasa amebakisha miezi miwili anawaambia haiwezekani.

Soma habari hapo Chini. Source; Mwanaspoti 22 jan 2015





YANGA imepanga kujenga uwanja wa kisasa wa mazoezi utakaoingiza watu 6,000 tu, lakini sasa inafanya mazoezi Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe, Dar es Salaam wenye vumbi na mabonde ili ikafanye vizuri dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wenye hali kama hiyo.


Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm, alilazimika kuhamishia mazoezi yake kwenye uwanja huo kutoka Boko Veterani ili wachezaji wazoee mazingira magumu kabla ya kuivaa Polisi Moro keshokuwa Jumamosi.

Pluijm alisema; "Tunakwenda kucheza na Polisi siyo mechi rahisi kwetu, tunaenda kukutana na mazingira mapya na kama inavyojulikana, uwanja tutakaochezea (Jamhuri) siyo mzuri, hivyo ndiyo maana tunafanya mazoezi hapa ili tupate matokeo mazuri."


Azam ina viwanja vitatu katika eneo lake la Chamazi ambavyo ni ule wa nyasi bandia, nyasi za kawaida na mwingine chakavu wenye nyasi kuukuu na mabonde. Timu hiyo hufanya mazoezi hayo katika uwanja wowote kulingana na uwanja watakaochezea mechi zao.


Wakati huohuo, Katibu wa Yanga, Jonas Tibohora, amekiri kuwa mchakato wa ujenzi wa uwanja mkubwa makao makuu ya klabu hiyo umeshindikana hivyo wamepanga kujenga uwanja huo mdogo wa mazoezi.

cc Makoye Matale Bantu lady mkolaj grafani11 sembo Deo Corleone The bos Amavubi Mdakuzi Pdidy Chakaza barafuyamoto nifah
 

Umetumwa na wezi sio? Imekula kwako.
 
Mhindi alidai wanachama walimfata agombee tena akagoma, hivyo wakaamua kumuongezea mwaka mmoja ili akamilishe mipango yake!!

Riz1 alipinga sana matokeo yake Mhindi akadai Riz1 si mwanachama, Prince Riz1 akatulia tuli!!
<Huwa najiuliza kama riz1 si mwanachama wa kandambili, Mhindi alimteua vipi kusimamia mradi wa ujenzi wa uwanja???>

Kila la kheri Mhindi katika kampeni yako ya kuwanyoosha kandambili.. na najua baada ya hiyo miezi 2, utaongezea miaka 2 ili ukamilishe ujenzi wa uwanja katika mkondo wa mto.
 
Manji usiondoke Mnyama mkali tuendelee kujipigia kimwana wetu kadri tutakavyo....
 
Manji tapeli mkubwa,kwanza kakamata wale wazee wasema ovyo wenye njaa,ule mpango wa kujenga Kaunda umefia wapi?,yupo pale kufanya biashara zake ziende na siyo kufanya Yanga isonge mbele....
 

Hahahahahh....umemwona katibu wao anawalaghai kuwa sasa mpango umebadilika

Sasa wanaenda kujenga uwanja wa mazoezi

Ule wa kuhama wakati wa mafuriko umeshindikana

Hhahaahhaha...chezea Kanjibhai wewe
 
Manji usiondoke Mnyama mkali tuendelee kujipigia kimwana wetu kadri tutakavyo....

Manji amawaweza sana wale jamaa

Anawageuza anavyotaka

Kama vile unavyokula samaki

Unageuza tu utakavyo wewe...hahahah
 
Hahahahahh....umemwona katibu wao anawalaghai kuwa sasa mpango umebadilika

Sasa wanaenda kujenga uwanja wa mazoezi

Ule wa kuhama wakati wa mafuriko umeshindikana

Hhahaahhaha...chezea Kanjibhai wewe

Sasa ndani ya miezi 2 utakamilika kweli? Huyu katibu pamoja na u dr wake anaonekana nae ni wale wale.
 
Ndio kazi ya mambumbumbu, kuchokonoa tu ya wenzao wakati ya kwao yanawashinda!
 
Ukitaka kumshambulia adui lazma ujue strength na weakness zake.. Na ndo mana tunapokutana na kandambili tunajua tuwashike wapi, then tunamaliza biashara mapema.
 
Sasa ndani ya miezi 2 utakamilika kweli? Huyu katibu pamoja na u dr wake anaonekana nae ni wale wale.

Hawa Yanga ni shida mkuu...sasa kanjibhai sijui ataondoka ndani ya hio miezi miwili au watampigia magoti tena
 
Atawajengea kama wa Loyola maana ndio wameuzoea.

Na kandambili huwambii chochote kuhusu uwanja wa loyola.. Ndo mana kabla ya mechi ya polisi ilibidi wahame uwanja, wakitafuta uwanja mbovu wenye hadhi ya jamhuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…