Utapeli wa nyumba unaoshika kasi Mbagala Chamazi na Chanika

Bila shaka nawe mjenzi wa nyumba uchwara
 
Kwani umeshauza ngapi[emoji23]
Sio nimeuza ngapi!!!?....umedanganya umma wa Watanzania! Unadhani serikali yako haioni ubora wa zile nyumba? Unafikiri wote wanaonunua zile nyumba ni Wajinga? Unadhani wanajenga bila vibali vya ujenzi? Na nikuhakikishie tu ndugu Nyumba hizi unazosema hazina ubora na hazina lenta na baadhi ya kuta hizo ni Uongo kabisa! Nyumba ni nzuri na zinauzika freshi tu tatizo mkishaanza kumiliki hizi smartphone mnakuwa waandishi wa Habari!
 
Ndugu Kicheche Mkali bila shaka mwenyewe ni jenga uza au dalali wa jenga uza ndio maana watetea ugali wenu.Vibali hailalishi ubora wa nyumba hiyo inayo jengwa ,iliyojengwa.Kwani hata utaratibu wa ukaguzi wa ubora haupo kwa sasa.Kipimo pekee ni vilio vya wauziwa nyumba zenyewe.Kwani hata Mashimo ya choo,jenga uza hachelewi kumuwekea chini ya sebule,urefu wenyewe akibahatika futi tanoπŸ€”
 
Hii sio kweli budah....
 
Wastaafu wanapata tabu sana[emoji23][emoji23] wametumikia nchi kwa jasho na damu, wanatapeliwa na Qnet, Mr. Kuku, DECI, AIM Global na sasa hivi kwenye nyumba[emoji16][emoji16]
Acha tu mnama yaani ni mabanzi juu ya mabanzi.
 
labda wamejengewa wasitaafu kutokana na life span yao
 
Halafu eti tuna "taasisi/mifuko ya wastaafu" inafanya kazi gani ilhali walengwa wao wanakuwa na maisha ya hovyo wakistaafu!!??
Kumuhifadhia mtu tu pesa zake sio lengo kuu la kuanzishwa kwa hiyo mifuko,bali ni kuhakikisha maisha yao baada ya kustaafu yanakuwa mazuri na salama.
Wastaafu wanapata tabu sana[emoji23][emoji23] wametumikia nchi kwa jasho na damu, wanatapeliwa na Qnet, Mr. Kuku, DECI, AIM Global na sasa hivi kwenye nyumba[emoji16][emoji16]
 
Mkuu unaweza kutuwekea nyumba mbili tatu za aina hio? Ambao watu walinunua na sasa hivi zimebomoka au kutoa nyufa?! Maanake hizi Stori tumesikia muda mrefu.
Fika Chanika mkuu,hizi nyumba zipo sana...
 
Hapo Dawa ya hili suala lipo kwenye Mikataba.
Sheria ya mauziano ya nyumba zipo, ambapo Serikali inatakiwa ishirikishwe na kodi ya TRA kulipwa.
-Sheria imetaja wazi haki za manunuzi na za muuzaji.
-Lazima muwekeane kipengele cha gurantee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…