Utapikaje maini yasiwe magumu

Utapikaje maini yasiwe magumu

CLONEY

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
104
Reaction score
29
Hivi utapikaje maini yasiwe magumu? Anaefahamu tafadhali anijuze.
 
Simple, anza kwa kuweka spice nusu saa kabla. Kisha kuyakaanga bila maji hta yakitoa maji mda unakaanga acha maji mpk yakaukie. Weka onion, green peper na carrot slice kaanga pamoja dk km 3 hivi. Malizia kwa kuweka soy sauce na vinegar au lemon. Yachanganye tena pamoja na hivyo vitu dk 3 zingine ipua kula yamotomoto-laiiinii
 
Yaunge moja kwa moja bila kuyachemsha,tia na vinegar itasaidia yabaki laini hata yakipoa!
 
Maini kuwa.magumu ni ishara ya kuwa overcooked. Fanya kama ulivyoshauriwa. Usiyachemshe kwanza. Ukiweka kwenye frying pan ama sufuria weka na mafuta kidogo ya kupikia na vitunguu.geuza hadi maji yenye damu yakauke. Then weka nyanya moja na spices, na chumvi. Weka vikorombezwo mboga mboga na utoe fasta.
 
...zaidi ya maelezo hayo hapo juu, unaweza pika kwa steam pia. marinade halafu yapike kwa mvuke for 5-7 mins. Kaanga vitunguu, nyanya, karoti na spices zako, tia ndimu halafu tia maini mwisho kabisa kwa dakika 2 epua
 
Weka maini kwenye frying pan ilio na mafuta kiasi maini yakiwa mabichi pamoja na vitunguu saum na tangawizi ya kutwanga kiasi na chumvi plus vitunguu maji kanga mpaka yaanze kuiva weka hoho na ndimu kiasi endelea mpk yaive kabisa it will take u just 10 to 15 min.
 
Back
Top Bottom