Ndugu wana JR nimeona mnisaidie kuteguwa kitendawili hiki cha aina gani ya wajumbe wa kamati ya maendeleo ya kata washiriki katika kuchagua mabaraza ya katiba ya wilaya kwa sababu suala la katiba ni la kitaifa kwa hiyo kulipaswa kufuatwa utaratibu mmoja katika kuwapata wajumbe hawa lakini inaonekana hakukuwa na utaratibu mmoja kwa nchi nzima kwa mfano Halmashauri ya wilaya lindi vijijini walioshiriki ni Madiwani na wenyeviti wa vijiji tu, Isitoshe wagombea hawakutakiwa kwenda kujieleza kwa wapiga kura wala hawakushirikishwa katika mchakato wa kuhesabu kura hizo na wala matokeo hawayajui. Sijui walioshinda ni nani?. Ukiangalia wajumbe walioshiriki kwa kila kata lindi vijijini ni WATANO KILA KATA. WAKATI kwa kawaida wajumbe wanaoshiriki katika vikao vya MAENDELEO YA KATA NI ZAIDI YA KUMI. NAO NI wakuu wa idara ndani ya kata, watendaji wa vijiji, watendaji wa kata, waheshimiwa madiwani , wenyeviti wa vijiji na viongozi wa dini. LAKINI KWA HILI KWA KUSHANGAZA NI KWAMBA HAWA WOTE HAWAKUSHIRIKISHWA ISIPOKUWA KWA MADIWANI NA WENYE VITI TU. JE hii ni sawa na ilitumika katika maeneo mengine? na kama si sawa walioshindwa wakakate rufaa wapi? Ninaomba jibu jamani.