Nilienda kijiji cha makonga wilaya ya newala 2010 kununua mbaazi hapo mtaani kulikuwa na mganga wa kienyeji mida ya saa 3 kasoro usiku tukapata taarifa kwa mganga kuna mgonjwa amefariki na huyo mgonjwa kwao ni mtama lindi,kila mwenye pikpiki wanaemstua abebe maiti anaogopa ikabidi hilo dili nilifanye niliwatoza elfu 90,sasa maiti nimeibeba kwa mfumo wa kumfunga kama huyo na nyuma akakaa mtu niliupiga mpini mpaka saa 7 usiku tunaingia mtama sasa kimbembe ni kwenye malipo yangu aisee mpaka kiasi kingine nilisamehe tu