A
Anonymous
Guest
UTARATIBU MBOVU WA UREJESHAJI ADA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM:
Nilifanya application ya kusoma evening program chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) college ya Journalism and Mass communication kwa mwaka 2023_24.
Nilipata admission lakini baadaye wakafuta program ya evening hivyo mimi na wenzangu ikatulazimu either kuhamia kwenye program ya full time, ku postpone mwaka au kuomba kurejeshewa ada.
Kutokana na sababu zilikuwa nje ya uwezo wangu ikiwemo mazingira ya kazini kwangu sikuweza kuwa na uchaguzi mwingine zaidi ya kuomba kurudishiwa ada.
Nilifuata taratibu zote za kuomba kurudishiwa ada kwa kuandika barua(hii ilikuwa mwezi December 2023). Majibu ya barua yangu yalitoka April 12 kwamba V.C amekubali nirudishiwe ada.
Lakini tangu majibu ya barua hiyo yatoke, nimekuwa nikizungushwa sana na ofisi ya uhasibu ya UDSM.
Mara ya mwisho waliniambia nisubiri mwaka wa fedha mwezi wa saba. Nikasubiri, mwezi wa saba ulipofika nikaenda kuuliza ikiwa wanaweza kunipatia hela yangu lakini wakanipiga tarehe hadi mwezi wa 10. Mwezi wa kumi umefika nikawafuata ofisi ya uhasibu tena kuwauliza wakasema niende chumba namba 201.
Kwenda kwenye hicho chumba 201 wanadai wao walishamaliza kazi bado tuu Barsar kuweka hela kwenye account. Nikirudi kwa barsar ananielekeza tena niende 201. Yaani kiufupi hawaonyeshi nia ya kurudisha pesa na wananisumbua mno kwa kunizungusha.
Gharama ambazo nimetumia kufuatilia suala hili zinaweza kufika laki 5. Na hapo kwenye pesa ambayo natakiwa kurudishiwa kuna hela wamekata kama laki moja na 35 elfu ambayo wanasema hawawezi kuirudisha, kiasi hicho ni pamoja na pesa ya dharura elfu 50 ambayo huwa ni refundable lakini wao wameizuia.
Naziomba mamlaka zinazohusika, ikiwemo wizara ya elimu kutusaidia tunaohangaikia refunds za ada chuoni UDSM maana inaonekana wanatuzungusha ili tukate tamaa wale hela zetu.