Utaratibu ukoje wa kufuta alama za vidole na kuondoa taarifa nilizotumia kusajili laini?

Utaratibu ukoje wa kufuta alama za vidole na kuondoa taarifa nilizotumia kusajili laini?

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Wakuu,

Baada ya kuchoshwa na usumbufu wa laini moja ya mtandao (kwa sasa sitaji jina la kampuni husika na laini hiyo), ambayo nimeisajili kwa taratibu rasmi zilizoelekezwa na TCRA; ninafikiria kwenda kuondoa/kufuta taarifa zangu nilizotumia kusajili laini hiyo kwenye kampuni mtandao husika.

Usumbufu niliokumbana nao ni huu:

1. Mara nne nimeenda kwenye kampuni ya mtandao niliyosajili laini hii ili wanifungulie laini baada ya kuifunga sijui kwa makosa gani. Na mara mbili nililazimika kuchukuliwa alama za vidole na mara mbili walifungua tu bila kuchukua alama za vidole.

2. Baada ya kukaa kama siku nne hivi bila shida na laini hii, Kwa sasa siwezi kutumia laini hiyo kupiga simu, kupokea sms, kuuliza salio liwe la muda wa maongezi ama la miamala ya fedha.

Nikipiga 100 kwa ajili ya kuomba msahada wa wahudumu wa mtandao, naambiwa maneno kibao ambayo kimuhitasari yanakuwa eti ' naweza kuwa nimevuka kiwango cha matumizi' na hapo wala hawanipi furusa ya kuuliza.

Wakishamaliza 'ngojera' zao wananikatia simu. Wakati huo, nimejiunga vifurushi viwili( internet na maongezi) vya mwezi, na mwezi haujaisha!!!

Usumbufu huu huu unajirudia hata nikipiga namba za watu wenye laini za mtandao huo ama za mitandao mingine.

3. Kwenye kupiga namba zile za kufuatilia masuala ya miamala ama malipo ya fedha, kwa sasa napata prompt messages ya "connection problems or invalid MMI code".

Kwa kufuata taratibu rasmi za IT, nimeenda kwenye sehemu ya ' mobile networks' kwenye ' setting section ' ya simu yangu.

Pale nimechagua 'Network mode' na kubadili mode ya LTE/3G/2G (autoconnect) kwenda 3G/ 2G autoconnect. Laini ikaonyesha kusoma mtandao yaani kialama cha 3G kikaonekana kwenye sehemu ya kuonyesha signal za mtandao.

Nilipojaribu kuangalia salio, Usumbufu namba 3 hapo juu ukajitokeza na hicho kialama cha 3G kikapotea.

Nikarudia zoezi hili kwa kubadili mode kwenda 2G only na kisha ile mode ya kwanza ya LTE/3G/2G(autoconnect) , usumbufu namba 3 bado ukajirudia.

Sikuchoka, nikiwa kwenye sehemu ya 'Mobile network', nikagundua ' network operators' inaonyesha ni mtandao huo ulioniuzia laini ya simu ndiyo upo active.

Nikiwa hapo hapo, nikachagua "Access Point Names", nikakuta ni mtandao huu ulioniuzia laini ndiyo upo active, na 'Name' yake imewekwa, (jina mtandao husika) internet, APN ( internet) na maelezo mengine.

Hapa sikubadili chochote. Lakini bado sipati internet wala siwezi kutuma sms, kupiga simu , wala kuuliza salio liwe la muamala ama la muda wa maongezi.

Kwa usumbufu huo, nimeazimia kwenda kufuta alama zangu za vidole kwenye mtandao huo na kufutwa taarifa zangu zote kutoka kwenye mtandao huo na laini yao kama watahitaji wanirudishie ela niliyonunulia.

Na kwenye kurudisha ela sitawadai fidia. Vinginevyo nitabaki na laini yangu kwa kumbukumbu za baadaye.

Sasa kabla sijatekeleza uamuzi huo, nikafikiri laweza kuwa jambo jema kupata muongozo wa utaratibu ni namna gani ninaweza kutekeleza hili kutoka kwa wakuu wa hapa JF.

Asante kwa kusoma maelezo yangu, na karibu kwa kunipa muongozo wa utaratibu ninaouhitaji.
 
mkuu nenda kwa ofisi zao utaratibu upo wa kufuta line istumike.
 
naona wadau wameususia uzi, anyway tuendelee kujuzana mkuu, mimi kuna mtandao mmoja wamekataa kupokea malalamiko yangu maana kila nikiwapigia kwa namba yao ya huduma naambulia kukaliwa kimyaa nampango wa kuwapiga chini na mimi pia nitawataka wafute taarifa zangu zote maana sitapata muda wa kuendelea nao.. over
NB. mtandao wenyewe ni ule wanatumia logo ya tone na pia wanatumia rangi nyekundu
 
Back
Top Bottom