KanaKansungu,
Inaonekana kwamba wewe bado hujaelewa taratibu za kupata hizo benefits.
Kwa nielewavo mimi ni kwamba unapata benefits zote kama wewe una uraia wa UK au "status" yako ni ile ya "indefinite leave to remain", kwamba uko "settled" hapa UK.
Benefit zote hizo zimeorodheshwa katika leaflet ya Inland Revenue ihusuyo benefits ambazo ni pamoja na child,housing,jobseekers na tax credits.
Unaweza kupata leaflet hii office yoyote ile kama ni London basi nenda pale Stratford-Broadway High Street au cental London pale Warren Street ofisi yao ipo chini ya jengo refu litazamalo Warren Street Station upande wa pili wa Euston Road.
Sasa kwa kifupi kama umekuja UK kukiwa mtalii inabidi usahau kuhusu kupata benefits yoyote ile kwani unakuwa upo hapa kwa muda mfupi na huruhusiwi kufanza kazi yoyote ile ya malipo (halali).
Kama upo UK ukiwa na viza ya uanafunzi basi kuna sehemu fulani ya mafao ambayo inabidi udai pale unapotaka kuondoka kurudi ulikotoka na maelezo yote utapata kupitia website ya HM Customs and InlandRevenue.
Hata hivyo pia kama upo hapa UK ukiwa na viza ya uanafunzi, huruhusiwi kudai benefits yoyote ile iwe child,housing au jobseekers na zingine kama taratibu za kupata hiyo viza zinavosema katika fomu zao za maombi.
Kwa hio kwa kuhitimisha natoa ushauri wangu kwako mheshimiwa kwamba ni pale tu unapokuwa na "settlement status" iwe "indefinite leave to remain" au "British Citizen" ndio utaweza kukaa ndani ya nyumba na kuvuta kila siku moja ya juma.
La unaweza kwenda hapa kwenye link ituatayo na usome zaidi.
http://www.hmrc.gov.uk/individuals/
Kila la kheri.