Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 363
Aisee kama kweli hiyo sio sawa,bora urudi tu nchini mwako!!!
'NO RECOURSE TO PUBLIC FUNDS' ni sentensi fupi tu ambayo inaonekana kwenye visa yangu, na to be frank, sikujali sana kutafuta maana ya maneno hayo miaka mitano iliyopita waliponigongea.Hii sentensi inamaanisha siwezi ku claim benefit, tax credit wala housing assistance. Jamani huu si unyonyaji? Ukizingatia wageni kama mimi tunatwanga mzigo kila siku, tena masaa kibao na kuna mizungu haifanyi kazi kabisa, inaishi kwa kutegemea hizo benefits tu, some of them have never done any paid work in their lives. Ni kama wanakula jasho letu tu, tax tunazolipa makazini ndo walipwa wao, huu nauona kama ubaguzi pia. So so unfair.
KanaKansungu,
Inaonekana kwamba wewe bado hujaelewa taratibu za kupata hizo benefits.
Kwa nielewavo mimi ni kwamba unapata benefits zote kama wewe una uraia wa UK au "status" yako ni ile ya "indefinite leave to remain", kwamba uko "settled" hapa UK.
Benefit zote hizo zimeorodheshwa katika leaflet ya Inland Revenue ihusuyo benefits ambazo ni pamoja na child,housing,jobseekers na tax credits.
Unaweza kupata leaflet hii office yoyote ile kama ni London basi nenda pale Stratford-Broadway High Street au cental London pale Warren Street ofisi yao ipo chini ya jengo refu litazamalo Warren Street Station upande wa pili wa Euston Road.
Sasa kwa kifupi kama umekuja UK kukiwa mtalii inabidi usahau kuhusu kupata benefits yoyote ile kwani unakuwa upo hapa kwa muda mfupi na huruhusiwi kufanza kazi yoyote ile ya malipo (halali).
Kama upo UK ukiwa na viza ya uanafunzi basi kuna sehemu fulani ya mafao ambayo inabidi udai pale unapotaka kuondoka kurudi ulikotoka na maelezo yote utapata kupitia website ya HM Customs and InlandRevenue.
Hata hivyo pia kama upo hapa UK ukiwa na viza ya uanafunzi, huruhusiwi kudai benefits yoyote ile iwe child,housing au jobseekers na zingine kama taratibu za kupata hiyo viza zinavosema katika fomu zao za maombi.
Kwa hio kwa kuhitimisha natoa ushauri wangu kwako mheshimiwa kwamba ni pale tu unapokuwa na "settlement status" iwe "indefinite leave to remain" au "British Citizen" ndio utaweza kukaa ndani ya nyumba na kuvuta kila siku moja ya juma.
La unaweza kwenda hapa kwenye link ituatayo na usome zaidi.
http://www.hmrc.gov.uk/individuals/
Kila la kheri.
Hapo ndipo utajua kwa nini LKJ alisema "Ingland is a Byach" kama hujaisikia hiyo record itafute.
Lakini uzuri ni kuwa hawakulazimishi, tafuta namna ya kuwa raia uweze ku claim benefit au kama la rudi nyumbani.Ukishindwa vyote kufa kisomi tai shingoni, banana nao humo humo na wanyime kivyako utakavyojua katika spending etc, unaweza kutuma remittance bongo watu wakujengee na kukuanzishia biashara halafu baada ya miaka michache unakipa.Haya yanakuwa ni maumivu ya muda tu ambayo ni necesary katika maandalizi ya maisha ya baadaye.
Sorry Kisura, I could have done better with the time it has taken me to respond to this. As far as I know, wanafunzi hawaruhusiwi kabisa kuclaim hizo benefits, mimi nafanya kazi na wafanyakazi wengi wenye Limited Leave to Remain pia hawaruhusiwi kuclaim japokuwa wanachangia kwenye tax na NI- ndio maana nadiriki kuiita system nzima 'unyonyaji'.To my understanding, hii kitu inaonekana sana ukipigiwa muhuri kama wewe ni "visitor" and/or "on transit". Nafikiri ukiwa hapo kama mwanafunzi, au unafanyakazi(legally)utakuwa na right to public funds! Au? Sasa mwenzetu wewe uko pale kama nani? I don't mean to pry, I'm just trying to get better understanding of the concern you have raised! Nisamehe kama nitakuwa nimekuudhi!
'NO RECOURSE TO PUBLIC FUNDS' ni sentensi fupi tu ambayo inaonekana kwenye visa yangu, na to be frank, sikujali sana kutafuta maana ya maneno hayo miaka mitano iliyopita waliponigongea.Hii sentensi inamaanisha siwezi ku claim benefit, tax credit wala housing assistance. Jamani huu si unyonyaji? Ukizingatia wageni kama mimi tunatwanga mzigo kila siku, tena masaa kibao na kuna mizungu haifanyi kazi kabisa, inaishi kwa kutegemea hizo benefits tu, some of them have never done any paid work in their lives. Ni kama wanakula jasho letu tu, tax tunazolipa makazini ndo walipwa wao, huu nauona kama ubaguzi pia. So so unfair.