Utaratibu wa chanjo usisubiri! Uanze sasa

Utaratibu wa chanjo usisubiri! Uanze sasa

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Nashauri kwa wale Watanzania watakaotaka kufanyiwa chanjo serikali iweke utaratibu na isisubiri mpaka wapate hizo chanjo.

Mfano wazee wa wahudumu wa afya wako hatarini zaidi basi waambiwe mapema utaratibu mfano kama vitambulisho vya taifa vitatumika ni vizuri wakajua mapema. Lakini vilevile serikali ingekuwa vizuri ijue wangapi wanataka chanjo na wangapi hawatataka ili waende kwenye group lingine la wenye magojwa sugu kama kisukari na pumu.

Familia nyingi wanajali zaidi wazee wao ambao wapo zaidi ya miaka 60 .

Tukitoa siasa mimi ushauri wangu binafsi nashauri ukiweza kupata chanjo usisikilize siasa mimi binafsi na ndugu zangu na watoto wao wengine kuanzia miaka 16 wamepata chanjo na hakuna aliyepata matatizo zaidi ya homa kidogo kwa siku moja au mbili.

Lakini wazazi wetu ambao wapo miaka 70 na 76 hawajapata chanjo bado Tanzania hivyo tunasubiri maana hizi chanjo wanauza kwa nchi sio hospitali binafsi hivyo hazipatikani mitaani kwa sasa.
 
Sasa kama wewe na familia yako mmepata chanjo na hakuna madhara mliyoyapata tulia sasa. Sisi hatutaki hiyo chanjo!

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom