Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Detention ilikuwa ni kwa watu threat tena wahaini siyo huu upumbavu unaofanyika sasa.Kwa Sisi wa kitambo kidogo wakati wa mwalimu sote tunaukumbuka utaratibu wa detention, ilikuwa endapo umeikera serekali basi kilichokuwa kikifanyika ni kukukamata kwa siri na kukuficha pahala, basi huko, utasoma magazeti, utasikiliza radio, utakula vizuri, kweli, lakini ulipo raia wa kawaida hawafahamu, basi utakaa humo weee, mpaka mamlaka ukiona sasa inatosha inakuachia, haikupeleki mbugani hapa, unaacha katikati ya jiji ghafla, uende zako!, kidogo kulikuwa na utu, hii piga, ua, toa macho, "" ahhaa ahhaa hapana, kwa kweli""
#Nimemalizia kwa lugha ya mpendwa wetu.
Detention ilikuwa kwa wote, wanaokera serekali ya wakati huo, wakiwepo wahaini,haya maroho ya kiuaji sijui yanatoka wapi!, unamwaga damu. Allah atunusuru.Detention ilikuwa ni kwa watu threat tena wahaini siyo huu upumbavu unaofanyika sasa.
Wahaini wa sasa hivi wapo ccm, wanapanga kuwa marais wakati kuna Rais madarakani mbona hawawapotezi hao wahaini waliopo ccm?
Well SaidDetention ilikuwa inafanyiwa watu wenye relevance, real threat na effect. Mf. Ndugai na Kapilimba.
Huu uhaini wa sasa hivi ni kama fungulia mbwa. Kwa wale wachache wenye madaraka wanatumia uuaji kama means ya kudhibiti 'threat' ambayo kiuhalisia haina formula maalum.
Ikiwa umemchukulia mwenye mamlaka demu wake na ukawa una vi followers elfu kadhaa kwenye social media basi unaangamizwa kwa kisingizio wewe ni 'threat'.
The real threat in all this ni mamlaka ya juu kabisa. Amehisi kuna uhalali wa watu wanaokinzana na sera/maslahi yake waangamizwe kupelekea kutengeneza loop hole ya watu kulipiziana visasi/kutesana/kutimiza dhamira zao mbovu.
In short kumetengenezwa kitengo cha 'hitmen' to be used by the highest bidder.
Sheria hiyo bado ipo, na ni mamlaka ya Rais tu.Kwa Sisi wa kitambo kidogo wakati wa mwalimu sote tunaukumbuka utaratibu wa detention, ilikuwa endapo umeikera serekali basi kilichokuwa kikifanyika ni kukukamata kwa siri na kukuficha pahala, basi huko, utasoma magazeti, utasikiliza radio, utakula vizuri, kweli, lakini ulipo raia wa kawaida hawafahamu, basi utakaa humo weee, mpaka mamlaka ukiona sasa inatosha inakuachia, haikupeleki mbugani hapana, unaachwa, katikati ya jiji ghafla, uende zako!, kidogo kulikuwa na utu, hii piga, ua, toa macho, "ahhaa ahhaa hapana, kwa kweli"
#Nimemalizia kwa lugha ya mpendwa wetu.
Kama ipo iboreshe na itumike, ni njema tu, na haitoi roho, haiumizi haiuwi, inafundisha kwa aina yake!Sheria hiyo bado ipo, na ni mamlaka ya Rais tu.
Au kuna ile ya kuzuiwa usitoke nje ya wilaya yako..
Wakati mwingine waliwahi kuhamishwa wakazi wa kijiji kizima toka mkoa mmoja kwenda mwingine!