Kidaya
Senior Member
- Dec 20, 2011
- 108
- 95
Mifuko ya pensheni ina jukumu muhimu katika kuhakikisha usalama wa kifedha wa watu kwa kutoa pensheni ya uzee, ulemavu na warithi, na mafao ya ugonjwa, kukosa ajira na uzazi. Tarehe 20 Oktoba, 2017 Serikali iliunganisha mifuko ya pensheni ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF na kuunda mfuko mmoja wa PSSSF kwa ajili ya watumishi wa umma na kuufanyia marekebisho mfuko wa NSSF uwe kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Mifuko ya pensheni inatumia utaratibu wa wanachama kuchangia kwa mwezi, ambapo michango inasimamiwa na mifuko na mwanachama anasubiri hadi atakapokidhi vigezo vya muda vilivyowekwa kulingana na pensheni au mafao anayostahili (mfano miaka 15 kwa pensheni ya uzeeni) ndipo apewe fedha zake kwa malipo ya mkupuo na ya kila mwezi.

Changamoto za utaratibu wa sasa
Utaratibu huu umekuwa na mapungufu mengi yanayokwamisha ufanisi wa mifuko ya pensheni hali inayosababisha malalamiko kwa wafanyakazi kama vile:
• Mlolongo mrefu wa wanachama kupata taarifa za michango yake kwa kulazimika kwenda ofisi za mfuko kuprintiwa taarifa zake
• Wanachama kutokuwa na uelewa wa kikotoo kinachotumika kwenye pensheni na mafao yake hivyo kutokujua kiasi cha fedha atakachopata
• Wanachama kutofaidikia na pensheni na mafao mengine yanayotolewa na mifuko kutokana na kutokujua au usumbufu wa ufuatiliaji
• Wanachama kutokuwa na taarifa wala maamuzi juu ya miradi inayofanywa na mifuko na atafaidika vipi na miradi hiyo.
• Mabadiliko ya kikotoo ya mara kwa mara yanayopunguza hela za mkupuo kwa wanachama kutokana na mifuko kuishiwa fedha
• Wanachama kupata fedha kidogo tofauti na matarajio yao hali inayowafanya wanachama kushindwa kutimiza malengo yao ya baada ya kustaafu kama vile ujenzi, malezi na uwekezaji.

Utaratibu wa hisa kwa mifuko ya pensheni na faida zake
Kwa sasa wanachama wa mifuko ya pensheni mfano PSSSF tunachangia 5% ya mshahara na mwajiri anachangia 15% jumla kuwa 20% ya mshahara. Utaratibu nwa hisa utatekelezwa kwa kuwa na bei ya hisa mathalani Tsh. 1000 kwa hisa moja, halafu michango ya mwezi ya mwanachama kugawanywa kwa bei ya hisa ili kupata idadi ya hisa anazomiliki na kuchangia mwanachama kila mwezi.
Utaratibu huu utakuwa na manufaa zaidi kwa wanachama na kuboresha ufanisi wa uendeshaji wa mifuko ya pensheni ya Tanzania kama ifuatavyo;
• Mapato zaidi kwa wanachama: Kuchangia michango ya kila mwezi kwa utaratibu wa hisa kunatoa uwezekano wa faida zaidi ikilinganishwa na uwekezaji wa sasa wa akiba ya kudumu. Wanachama watafaidika na ongezeko la mtaji na mapato ya gawio la faida ya kila mwaka, ambayo yataongeza mapato na faida kwa wanachama.
• Kuwa na maamuzi juu ya uwekezaji unaofanywa na mifuko ya pensheni: Utaratibu wa hisa unawafanya wanachama kuwa wamiliki wa mifuko ya pensheni hali inayowapa nafasi ya kuhudhuria vikao vya mkutano mkuu inayojadili maendeleo ya mifuko ikiwemo miradi inayotaka kutekelezwa na mifuko. Kwa sasa mifuko inaanzisha miradi mikubwa bila idhini ya wanachama, na miradi hii ikikwama au kupata hasara mwanachama hujikuta wakibeba hasara hizo kwa kubadilishiwa kikokotoo ili kuwapunguzia fedha wanazopokea.
• Kuongezeka kwa maarifa ya kifedha: Kuruhusu wanachama kuchangia kwa njia ya hisa kutawapa wanachama maarifa zaidi ya kifedha na hisa ili kufanya maamuzi sahihi kuhusu uwekezaji wao. Maarifa haya yaliyoongezeka yanaweza kusababisha mipango bora ya kifedha na udhibiti wa akiba yao.
• Kutoa fursa za mikopo kwa wanachama: Utaratibu wa hisa utatoa fursa kwa wanachama kukopa kulingana na idadi ya hisa zao ili wapate fedha za kufanyia shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile ujenzi, biashara au hata kujigharamia masomo.
• Kutoa fursa za kuuza na kununua hisa: Utaratibu huu utawawezesha mwanachama kuuza hisa endapo anaona ana uhitaji unaomlazimu kufanya hivyo mfano upotevu wa ajira/mapato, dharura mbalimbali. Pia mwanachama apata fursa ya kununua hisa ili kuongeza akiba yake na hatimae kujiongezea faida zaidi ya mgawo na mikopo.
• Kuwa na viwango tofauti vya uwekezaji: Utaratibu wa hisa utawapa wanachama uwezo tofauti wa kuweka akiba kulingana na uwezo wake wa kifedha mwezi hadi mwezi. Utaratibu wa sasa wa kuchangia 5% unamnyima fursa mwanachama kuweka zaidi endapo amepata fedha za ziada kutoka kwenye vyanzo vingine kama posho za safari, biashara na uwekezaji wake.
• Usimamizi bora wa mifuko: Utaratibu wa sasa wa menejimenti na bodi za mifuko kuwa ndio waamuzi wa msuala yote ya kiuendeshaji unatoa mwanya wa ubadhirifu na uwekezaji usio na tija kama tunavyoshuhudia miradi mingi ya mifuko isivyo na tija au ina ufanisi mdogo tofauti na matarajio. Utaratibu wa hisa utawaongeza wanachama wote kuwa wasimamizi hali itakayoimarisha utendaji wa mifuko.
• Ukuaji wa mtaji wa mifuko: Utaratibu wa hisa utaiwezesha mifuko ya pensheni kukuza mitaji kwa haraka zaidi kutokana na wanachama kuwa na fursa ya kununua hisa kadri ya uwezo wao hivyo mifuko kuwa na nguvu zaidi ya kuwekeza hali itakayosababisha faida za juu na mafao makubwa ya kustaafu kwa wanachama.

Mambo ya kuzingatia ili kufanikisha utaratibu huu
Utaratibu wa hisa utaweza kufikia faida tajwa kwa kuzingatia yafuatayo;
• Kuwaelimisha wanachama kuhusu faida na hatari za kuwekeza kwenye hisa kuwaongezea wanachama uelewa wa masuala ya kifedha ili wafanye maamuzi sahihi ya uwekezaji wao.
• Mfumo imara wa kisheria ni muhimu katika kuhakikisha uwazi na uadilifu wa uwekezaji wa mifuko ya pensheni ili kulinda na kuzingatia maslahi ya wanachama na kutoa usimamizi ili kuzuia shughuli za ulaghai na ubadhirifu katika mifuko.
• Kutumia mifumo ya kidigitali (website na apps) kutapunguza usumbufu na gharama za fedha na muda kwa wanachama wanapotaka taarifa za hisa na akiba zao wakati wowote mahali popote.
• Masoko ya hisa yana tabia ya kuyumba, na mabadiliko ya muda mfupi yanaweza kuathiri thamani ya uwekezaji. Mifuko ya pensheni inahitaji kuendeleza mikakati ya kudhibiti kuyumba huku, kama vile kuweka malengo sahihi ya uwekezaji.
• Ushiriki wa kikamilifu na kujitolea kutoka kwa wanachama ni muhimu kwa mafanikio ya mbinu hii. Mifuko ya pensheni inapaswa kuwahimiza wanachama kutathmini mara kwa mara chaguo zao za uwekezaji na kufanya marekebisho kulingana na malengo yao ya kifedha na hali ya soko.
Wanachama kuchangia michango yao ya kila mwezi kwa utaratibu wa hisa za kila mwezi kutatoa manufaa makubwa na kuboresha uendeshaji wa mifuko ya pensheni nchini Tanzania.

Upvote
12