Utaratibu wa kufungua kituo cha mafuta ukoje?

KingCobra95

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
3,249
Reaction score
5,863
Moja moja niende kwenye mada, naomba kuuliza utaratibu wa kufungua sheli ukoje?

Nahitaji vibali kutoka taasisi ipi na ipi? Na je inaruhusiwa kufungua sheli katikati ya makazi ya watu?

Nauliza hivi kwasababu kuna sheli nimeiona njia ya kuelekea chuo kikuu UDSM kule Ubungo Msewe ipo katikati ya makazi ya watu.

Je hii sio hatari kwa usalama wa watu.?

Najiuliza mengi mf. malori yanayofanya refueling yatapita njia gani na nguzo za Tanesco ziko chini chini kabisa..
 
Siku hizi hakuna hizo sheria mkuu...imagine kiwanda tena cha pombe kali kinapakana na nyumba za makazi yaani mpaka harufu ya pombe inaingia mpaka kwenye nyumba za watu hapo unategemea watoto wa mazingira hayo afya zao zitakuwaje baada miaka mitano tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…