Utaratibu wa kukagua magari kurudi kama zamani

Utaratibu wa kukagua magari kurudi kama zamani

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Mhe. Rais tunakushukuru kwa tamko lako kuwa ukaguzi wa magari utarudi kama zamani. Naomba amri hii ingeanza hata leo.

TBS wamekuwa wanatumia nafasi zo vibaya kwa kuwatesa wananchi wanapofuata magari yao Bandarini.

Asilimia karibu 98 ya wateja hawajatoka bure bila kuambiwa kuwa gari yako ina kasoro na baada ya kuambiwa hivyo lazima ujiongeze.

Kwa kweli wametesa sana wateja. Fedha ambazo zimeingia mifukoni mwao tangu utaratibu huu uanze zinaweza kujenga vituo vya Afya hata mia moja.
 
Kwa hili hakika Muheshimiwa Rais ameupiga mwingi, watu walikua wanalia, wengine Hadi leo hii wanatembelea Chassis Number, kwa kunyimwa certificate na kushindwa kusajili magari Yao . Ilikua ni shida kwelikweli, Kila gari itakayoingia bandarini utaambiwa mara tyres, mara engine lickege , Yani ilikua ni pesa pesa tu. Asante sana kwa uamizihuu, tutapumua sasa.
 
Hili swala tulilipigia kelele sana, iweje magari yasikaguliwe huko yanakotoka yaje kukaguliwa hapa.........kumbe kuna watu walitengenezewa ulaji, mambo mengine yanayofanyika nchi hii ni ya hovyo sana.......
 
Mhe. Rais tunakushukuru kwa tamko lako kuwa ukaguzi wa magari utarudi kama zamani. Naomba amri hii ingeanza hata leo.

TBS wamekuwa wanatumia nafasi zo vibaya kwa kuwatesa wananchi wanapofuata magari yao Bandarini.

Asilimia karibu 98 ya wateja hawajatoka bure bila kuambiwa kuwa gari yako ina kasoro na baada ya kuambiwa hivyo lazima ujiongeze.

Kwa kweli wametesa sana wateja. Fedha ambazo zimeingia mifukoni mwao tangu utaratibu huu uanze zinaweza kujenga vituo vya Afya hata mia moja.

Walifanya fursa kwa hakika wasiachwe tu - wafilisiwe
 
Mhe. Rais binafsi ninashauri umuwajibishe Director General wa TBS. Yeye alikuwa anajua mchezo mzima na kwa nini hakuwachukulia hatua wafanyakazi waliokuwa wanafanya mchezo huu. Nchi hii sijui tuna matatizo gani.
 
Kimsingi serikali ilitakiwa iweke specifications zinazotakiwa za ubora wa magari, halafu wauzaji wa magari kule japan wafanye ukaguzi kwenye karakana zao zinazotambulika kisheria kwa kuzingatia vigezo vya ubora vinavyohitajika Tanzania na kupewa certificate ambayo wataiambatanisha na gari linapokuja. Sasa mamlaka za Tanzania zinatakiwa zipitie tu hiyo certificate ya ukaguzi kujiridhisha kwamba ukaguzi ulifanyika kwenye maeneo fulani na fulani yaliyoainishwa na kukidhi vigezo na hapo ndo inakuwa imeweka tozo kwa ajili ya uhakiki. Vinginevyo serikali itaishia kuwatengenezea wajanja wachache ulaji huku yenyewe isipate chochote na wala malengo yake yasitimie.​
 
Magari yakaguliwe kule kule yanakotoka kama zamani, wajapani hawana longo longo wanachotaka soko lao lisife tu hawawezi kuuuza bidhaa famba , long time nikiwa bongo niliwahi kuagiza gari kwa inspection ya JAAi huko japan yani gari supa wala haikusumbua for more than 7 years, sasa hawa wakwetu rushwa inatoka lakini migari bado mibovu , wakatyi mwingine gari nzima watu wanalazimishwa rushwa yani vurugu tu
 
Tbs Hakuna wanachosaidia gari bovu unawapa rushwa linakuwa zima , bora raisi kaliona hili. Hao TBs watuambie ni jumla ya magari mangapi wameyarudisha yalipotoka sababu ya ubovu
 
Back
Top Bottom