Ndugu wadau wa elimu,
Tunafahamu kuwa kazi ya kutoa huduma ya elimu nchini Tanzania inafanywa na serikali na sekta binafsi. Serikali inajukumu la kuandaa sera, mitaala na kutoa miongozo kuhusu namna bora ya kutoa elimu ya msingi na sekondari. Shule zote za skondari nchini(shule binafsi na za serikali) zinawajibu wa kufuata miongozo ya serikali katika utoaji elimu. Miongoni mwa malelekezo ambayo shule binafsi za sekondari zinapaswa kufuata ni kukaririsha darasa wanafunzi wa kidato cha pili wanaoshindwa kufikia wastani wa alama 30 katika mtihani. Nijuavyo mwanafunzi akishafaulu kidato cha pili halazimiki kurudia darasa; ataendelea hadi atakapofanya mtihani wa kidato cha nne.
Kwa makusudi au kwa kutokujua shule binafsi za sekondari zimekuwa na tabia ya kuwalazimisha wanafunzi kukariri madarasa baada ya kushindwa kufikia wastani wa shule ambao ni kinyume na maelekezo ya wizara ya elimu; Mfano katika shule A mwanafunzi anatakiwa afikie wastani wa alama 50 ili aendelee kidato kinachofuata.... Vinginevyo analazimika kuhamishwa shule nyingine ambayo itamkubali. Kumkaririsha mtoto shule kunawafanya wazazi kuingia gharama ambayo ingeweza kumsaidia mtoto katika ngazi ya juu ya elimu. Pia utaratibu huu unampotezea muda mtoto au hata kumkatisha tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari
Ndugu wadau, Je, serikali imeshindwa kuzisimamia shule binafsi za sekondari?
Je, nini kifanyike ili kuwaondolea adha wazazi na watoto?