Utaratibu wa Kukariri darasa shule binafsi unaumiza wazazi/walezi na watoto

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
Ndugu wadau wa elimu,

Tunafahamu kuwa kazi ya kutoa huduma ya elimu nchini Tanzania inafanywa na serikali na sekta binafsi. Serikali inajukumu la kuandaa sera, mitaala na kutoa miongozo kuhusu namna bora ya kutoa elimu ya msingi na sekondari. Shule zote za skondari nchini(shule binafsi na za serikali) zinawajibu wa kufuata miongozo ya serikali katika utoaji elimu. Miongoni mwa malelekezo ambayo shule binafsi za sekondari zinapaswa kufuata ni kukaririsha darasa wanafunzi wa kidato cha pili wanaoshindwa kufikia wastani wa alama 30 katika mtihani. Nijuavyo mwanafunzi akishafaulu kidato cha pili halazimiki kurudia darasa; ataendelea hadi atakapofanya mtihani wa kidato cha nne.

Kwa makusudi au kwa kutokujua shule binafsi za sekondari zimekuwa na tabia ya kuwalazimisha wanafunzi kukariri madarasa baada ya kushindwa kufikia wastani wa shule ambao ni kinyume na maelekezo ya wizara ya elimu; Mfano katika shule A mwanafunzi anatakiwa afikie wastani wa alama 50 ili aendelee kidato kinachofuata.... Vinginevyo analazimika kuhamishwa shule nyingine ambayo itamkubali. Kumkaririsha mtoto shule kunawafanya wazazi kuingia gharama ambayo ingeweza kumsaidia mtoto katika ngazi ya juu ya elimu. Pia utaratibu huu unampotezea muda mtoto au hata kumkatisha tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari

Ndugu wadau, Je, serikali imeshindwa kuzisimamia shule binafsi za sekondari?
Je, nini kifanyike ili kuwaondolea adha wazazi na watoto?
 
Kwa hiyo sababu alifaulu Form II hata akipata wastani wa 12 Form III aendelee? Mi naungwa mkono kanuni ya kwamba mwanafunzi atavuka darasa kwa wastani usiopungua 50.
 
Kwa hiyo sababu alifaulu Form II hata akipata wastani wa 12 Form III aendelee? Mi naungwa mkono kanuni ya kwamba mwanafunzi atavuka darasa kwa wastani usiopungua 50.

Ni utaratibu wa serikali kuwa kutakuwa na mtihani wa mchujo kidato cha pili tu. Je, shule binafsi zinachuja wanafunzi kila kidato kwa kufuata maelekezo ya nani? Na kama mtoto alifaulu kidato cha pili atawezaje kupata 12? Je, walimu wa shule binafsi za sekondari wanazo sifa? wanatekeleza wajibu wao wa kufundisha? kama wanafundisha kwa nini watoto wanafeli? kama mtoto hana bidii katika masomo, je, wanamshirikisha mzazi? au wanachukua hatua gani ili mtoto apate elimu bora?
 

Huo ni muongozo tu na unaweza boreshwa zaidi. Ni vema serikali iweka kanuni kwamba kila kidato mwanafunzi avuke kwa walau C. Hali ni mbaya mkuu, hizo siasa za kwamba serikali ndio imeweka na wengine hawana utashi wa maboresho ni batili. We angalia elimu yetu jamani! angalia mazalisho ya vyuo vikuu, wanafunzi wanamaliza wengi. Statistic zimepanda lakini je wanaweza tetea hizo degree zao? Ubora wa elimu yetu Tz jamani? Mungu ibariki Tanzania
 
Utapata gharama kubwa endapo mwanao atakuwa hajishughulishi kwa bidii na masomo,ili kuondoa hasara hii!msisitize mwanao asome kwa bidii,kama haiwezekani,mpeleke shule za kata akajiachie, afeli ili wewe na yeye mkagharimike zaidi!
 
Jamani tuache mawazo hayoo! Sasa itakuwa mtu akipata wastani wa kumi aende tu? Ukiona shule hiyo ujue ghalama atakapo feli form 4 ni kubwa zaidi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
ukiona elimu ni gharama jaribu ujinga ,mtoto anayepata division four form four ni janga kwa wazazi ni bora arudie mpaka awe vizuri
 
Uyo mwanao lazima atakuwa amerithi akili zako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…