Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole sana ndugu kwanza ntakwambia kuwa ardhi yote ya taifa hili ipo chini na uangalizi wa rais na kwa maana nyingine kiujumla mamlaka ipo kwa serikali.
Sasa nataka kujua hiyo ardhi uliipataje!?
Ardhi hii ilipatikana baada ya serikali ya kijiji kuombwa shamba ambalo kuna mtu alipatiwa na baada ya muda akashindwa kuliendesha akaamua kuliuza kwangu. Tulipokuwa tukiuziana tulifika kijijini ni na kuuona uongozi wa kijiji na wakawa ,mashahidi wa mauziano yetu.
Je una vibali (ushahidi) vya miliki ya hiyo ardhi!?
Serikali ya kijiji ilitoa barua yenye kueleza ukubwa wa shamba na
Pindi shamba lako linachukuliwa ulikuwa nje ya milki yako kwa mda gani!?
ninalo kwa miaka 2 lakini lina miaka 5 tangu limetolewa
Je ulishapewa taadhali kutoka serikalini kuhusiana na uchukuzi wa ardhi yako!?
hawajatoa taarifa za maandishi kwa uamuzi huo
Je ushaambiwa madhumuni au lengo au sababu ya kuchukua shamba lako!!?
Mwenyekiti na mtendaji wanasema wamechukua mashamba hayo kwasababu hayajaendelezwa
katika kila swali nimeweka majibu husika nisaidie mkuu
Hapa sasa nadhan tunawrza kwenda pamoja na wadau wengine wanaweza kusaidia hapa.
Kama mauziano.ya ardhi yalikuwa ya halali nadhani wewe tayari n mmiliki husika wa hilo eneo.
Kama hoja ni kuchukua hiyo ardhi kisa haijaendelezwa aomba uweke wazi hapa shamba lako tangu umenunua umefanya shughuli gani za kimaendeleo katika hilo eneo!?
Upande wa serikali ya vijiji hawajafuata taratibu ya kukupa kibali cha nia ya kunyanganya ardhi na hiyo ni ukiukwaji wa taratibu na tendo hilo linaweza kukupa ahuweni lakini naomba ujibu kwanza swali hapo juu!!