Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema watu wenye tabia ya kuunga mkono kila wakati ni wasaka fursa na hawana msaada wowote katika nchi.
Kipindi cha miaka mitano iliyopita tumeona tabia hii ya kusifia kila kitu ikikomaa na kufikia kiwango cha juu kabisa nchini. Hali hii ileletwa na utamaduni ambao haukwa mpya sana tofauti na awamu nyingine ila kwa kipindi hiki ulishika kasi zaidi. Utaratibu huo ni wa watu walio nje ya utumishi wa serikali au vyama vyao wengine wakiwa hawana sifa kabisa kuteuliwa katika nafasi za utumishi.
Matokeo yake tumekuwa na kundi kubwa la wasifiaji 'praise team' kuanzia kwa vijana wadogo kabisa wanaomaliza vyuo hadi wazee wanaotakiwa kucheza na wajukuu zao tu. Na hali ni kwa kila sekta nchini, iwe vyuoni, polisi, bungeni, makanisani, misikitini, vyombo vya habari hadi hapa JF!
Serikali mpya inatakiwa idhibiti hali hii ili taifa letu lisizidi kuwa la hovyo. Nafasi za juu na nyingine zozote katika utumishi wa umma zipatikane kwa watu kupanda madaraja katika taaluma, sekta na idara zao husika. Serikali na vyama vya siasa visitishe utaratibu wa kuokoteza watu kokote waliko na kuwapa majukumu ya kiutumishi. Nafasi za kiutumishi zipatikane kwa kupanda ngazi. Watumishi wapande ngazi kuanzia ya chini kabisa.