Mimi nina nyumba Chanika jirani yangu anasema nimeingia kwake upana wa nyumba yangu 45 mt lakini nikipima ni 42 mt bado anasema nimejenga kwake. Je, utaratibu upoje wa kupata watu wa ardhi waje wapime watuwekee becon kila mmoja ajue mipaka yake na gharama ngapi? Mwenye kujua naomba anafafanulie.
Kwanza kabisa lazima ujue mambo mawili, mosi; unataka kupimiwa na Halmashauri au unataka kupima na Mtaalamu binafsi. Ukishatambua hayo ndio inakwenda kwenye zoezi lenyewe la kupima kwa mujibu wa Sheria.
1) Utaratibu unaanza kwa kuanzika barua kupitia serikali yako ya Mtaa na Kata kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri yako ukieleza nia yako ya kupima eneo lako. Barua hii haitozwi gharama yoyote kwa maeneo mengi.
2) barua hiyo lazima ianishe unataka kupima na nani. Kupima na Mtaalamu binafsi lazima umtaje katika barua hiyo na awe na vigezo vya kufanya kazi hiyo kwa.mujibu wa Sheria. Na kama unataka kufanya na Halmashauri pia elezea nia hiyo kwenye barua yako.
3) Wataalam watachukua taarifa za awali(majira ya nukta) ili kufanya utafiti wa awali, ikiwa eneo limepimwa/au halijapimwa au kama eneo liko ndani ya mpango wa matumizi ya Ardhi au bado.
Ikiwa eneo liko ndani ya eneo la mpango inakupunguzia sehemu kubwa ya gharama, ikiwa liko ndani ya mpango ila halijakaa kulingana na mpango basi gharama za marekebisho ya mpango hazina tofauti na gharama za kuandaa mpango mpya kwa maeneo mengi..na shughuli hii hufanywa na Mtaalamu wa mipango miji aliyesajiliwa na bodi ya Wataalam wa mipango miji TPRB.
4) Ukishapata mpango, aidha kwa kuandaa, au kuurekebisha au kukuta umekwisha kuandaliwa, hatua inayofuata ni ya kuweka alama(vigingi) uwandani (unaojulikana kwa wengi kama upimaji) na kazi hii hufanywa na surveyor. Na baadae kuwasilisha katika ofisi za ardhi mkoani kwa uidhinishaji.
NB;
a) Kwa sasa uko mfumo mpya wa kuwasilisha kazi za upimaji, unaojulikana kama Tariff-11 hakikisha mtaalamu unayemkamisheni kazi yako anaufahamu mfumo vizuri la si hivyo mtaanza kufukuzana kama kuku na fedha ameshakula.
b) Kupima ni Pamoja na Kupanga matumizi ya Ardhi, kuweka alama ardhini na kutengeneza sheria ndogo maalumu za uendelezaji wa maeneo.