Uchaguzi 2020 Utaratibu wa Kupiga Kura na kura zilizoharibika

Uchaguzi 2020 Utaratibu wa Kupiga Kura na kura zilizoharibika

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Utaratibu wa Kupiga Kura

(i) Mpiga Kura atatakiwa kwenda na Kadi yake ya kupigia Kura Kituoni na kumpa Msimamizi Msaidizi Na. 1 wa Kituo;
(ii) Msimamizi Msaidizi Na. 1 wa Kituo atasoma kwa sauti jina la Mpiga Kura ili kuwawezesha Mawakala kuangalia taarifa za Mpiga Kura huyo katika Daftari la Kituo;
(iii) Msimamizi Msaidizi Na. 1 wa Kituo ana haki ya kumuuliza Mpiga Kura swali lolote linalohusiana na utambulisho wake iwapo ana shaka naye;
(iv) Msimamizi wa Kituo kabla ya kumkabidhi Mpiga Kura Karatasi za Kura atagonga Muhuri wa Kituo;
(v) Msimamizi wa Kituo atampatia Mpiga Kura Karatasi ya Kupigia Kura na kumuelekeza namna ya kuikunja Karatasi hiyo baada ya Kupiga Kura;
(vi) Mpiga Kura atatakiwa kwenda katika Kituturi na Kupiga Kura yake kwa siri;
(vii) Mpiga Kura atatakiwa kuweka alama ya vema (√) katika eneo la Mgombea ambaye anamtaka katika Karatasi ya Kupigia Kura;
(viii) Mara baada ya Kupiga Kura, Mpiga Kura atazikunja/ataikunja Karatasi yake ya Kura na kuitumbukiza katika Sanduku la Kura lililowekwa katika eneo la wazi la Kituo; na
(ix) Kabla Mpiga Kura hajaondoka Kituoni anatakiwa kupakwa Wino Maalum na Msimamizi Msaidizi Na. 2 wa Kituo katika Kidole Kidogo cha Mwisho cha Mkono wa Kushoto

Kuharibika kwa Kura

Karatasi ya Kura haitahesabiwa kuwa Kura Halali iwapo Kura hiyo:-
(i) Haina Muhuri wa Kituo;
(ii) Imepigwa kwa Mgombea zaidi ya mmoja;
(iii) Ina alama, au maandishi yanayoweza kumtambulisha mtu aliyepiga Kura;
(iv) Haina alama yoyote; na
(v) Amepigiwa Mgombea aliyejitoa.
 
Upvote 0
Kuna ujanja ujanja umefanywa na tume mwenye karatasi ya kura.
 
Tuambie huo ujanja ujanja mkuu ili tuwe aware nao..
1. Ile karatasi ya kupigia kura kwa jinsi ilivyoketwa (sample) haijafuata utaratibu unaotakiwa, hiyo ni janja namba moja.

2. Siku ya kupiga kura unaweza shangaa ukaletewa karatasi iliyofuata utaratibu wa ki_alfabeti ili kukuchanganya mpiga kura.


3. ....
 
ALAMA ZINAZOKUBALIKA KATIKA KARATASI ya Kura
Alama inayokubalika katika kupiga kura ni alama ya vema (√) lakini
iwapo mpiga kura atashindwa kuweka alama hii kama inavyotakiwa,
alama yoyote inayoonesha wazi kwamba mpiga kura alitarajia kumchagua
nani ikubaliwe.
Alama hizo ni pamoja na 'X', ili mradi tu iwe katika chumba kilichopo
wazi. Kama mpiga kura atashindwa kuweka alama katika chumba
kilichopo wazi na badala yake akaweka alama hiyo kwenye jina la
mgombea au chama chake, alama hiyo inakubalika na ni kura iliyo halali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom