Utaratibu wa kutoa talaka upoje?

danhoport

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
1,984
Reaction score
4,502
Kwema humu,

Nisiwachoshe nimeishi na mke wangu kwenye ndoa mpaka sasa ni miaka mitano ila kutokana na changamoto za ndoa nilikuwa nahitaji tuachane kwa amani na mke wangu pasi kugombana, kwahiyo nilikuwa nahitaji kumpa talaka.

Msaada wenu taratibu za kuandika talaka upoje?
 
Kama ni muislam nenda bakwata wilaya. Kama ni mkristo nenda kanisani au ofisi ya kata kwanza.

Kama hamna mali huna haja ya talaka we beba suruali zako jiondokee.

Kwa wakristo talaka ni kwa matajiri ili wagawane mali kisheria sasa weww kapuku talaka ya nini.

Nb talaka huandiki wewe inaandikwa na hakimu based on your grounds za kuachana
 
Upo tiyari kukaa bila kuoa tena mpendwa? Kumbuka kuachana ni machukizo kwa Mungu!

Malaki 2:16
Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
 
Ni muislmu
 
Nikitoka nimetoka, sirudi tena
 
Acha kutisha watu kwa vijiquotesheni vya kuunga unga,wazungu wamepotosha sana ninyi, kwahiyo ni bora wauane kwenye ndoa kuliko kuachana au??

Wazungu wenyewe wanasema ndoa ni ya mke na Mme, hapo hapo wanapigia chapuo ndoa za jinsia moja na ndo hao hao walileta huo upuuzi wa mke mmoja!!

Men are polygamous in nature
 
Habari Mkuu
Kuna vitu muhimu vya kufahamu hasa linapokuja swala la talaka kwani watu wengi hudhani talaka ni jambo la wanandoa pekee, si kweli.

1. Talaka hutolewa na Mahakama, hivyo ili kupata talaka ni lazima ukafanye maombi Mahakamani na si kila Mahakama bali itakupasa kuzingatia maelekezo ya sheria kulingana na aina ya ndoa yenu

2. Talaka hutolewa kwa kuionesha Mahakama sababu za msingi za kuifanya iamini kuwa ndoa yenu hioyo hairekebishiki tena. Fahamu kuwa Mahakama yenyewe haipendi kutoa talaka/kuvunja ndoa za wapendanao.

3. Talaka itakupa uwezo wa kutambulika kama mtu asiye ndani ya ndoa, hii ina maana kuwa kwa wakristu wataweza kuoa/kuolewa tena na kwa waislamu itahesabu ongezeko la idadi ya nafasi ya kuoa mke mwingine, kwa watamaduni vivyo hivyo pia.

4. Talaka hutolewa kwa ndoa inayotambulika kisheria na ili kuthibitisha uwepo wa hiyo ndoa ni sharti pawepo cheti cha ndoa hiyo. Hii ni kwa ndoa za aina zote, kidini, kiserikali na kimila, ni sharti ndoa iwe imesajiliwa kwa msajili wa ndoa.

5. Kabla ya kufanya maombi ya talaka Mahakamani ni sharti muwe mmeshapita kwenye usuluhishi wa ndoa, na ikashindikana kusuluhishwa hivyo mkapatiwa hati ya kushindwa kwa usuluhishi. Usuluhishi unaweza kufanywa na Baraza la kata au mabaraza ya kidini ya usuluhishi wa ndoa, ila sharti Baraza hilo liwe linatambulika kisheria.

6. Baada ya talaka kinachofuata ni mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja, hapa ni lazima ijulikane kuwa huu mgawanyo una wahusu watalaka pekee na wala hauwahusu watoto wao. Kumekuwa na mazoea na dhana kwamba mali tutawapa watoto, hii ni kinyume na sheria. Zipo kesi za Mahakama Kuu zilizopinga hili swala/mtazamo.

Mwisho kabisa, pole kwa maswahibu Mkuu, pima uzani wa unayopitia kisha tafakari vizuri kama kweli talaka ndjo suluhisho la hayo maswahibu. Ukiona ndio basi fuata utaratibu, ukikwama unaweza niuliza siku yoyote nitakupa mwanga pindi nitakapoona swali lako.

Kila la kheri.
 
Katika Uislamu kuna talaka za aina nyingi! Kwa maelezo yako unataka uachane na huyo mwanamke

Unaweza kumtamkia maneno tu yakatosha kuwa talaka na kuanzia hapo hutakiwi kumgusa maana kufanya nae tendo unaitengua ile talaka kabla ya kipindi cha eda kuisha.

Au unaweza kumpa talaka kwa maandishi ya kumuandikia hapo tayari hyo talaka ni halali katika dini.

Baada ya kipindi cha Eda kumalizika pasi kumgusa , huyu mwanamke anakuwa sio halali yako tena na kama ukihtaji kurudiana nae mnatakiwa muaze process za barua , mahari mpk ndoa tena.

kama mna mali basi utafungua shauri bakwata kwa ajili ya mgawanyo wa mali lakini kama kapuku mpe karatasi yake ya talaka beba suruali zako anza maisha upya hiyo ni talaka tayari kwa Mujibu wa dini.
 
Nimekuelewa ndugu, ngoja nimuandikie mana tayari nishamtamkia
 
Ni muislmu
Waislamu mahari huwa ndogo na ndoa hudumu muda kidogo

Mwanaume au mwanamke wa kiislamu kuomba talaka ni kitu kidogo tu

Ndoa za Kikiristo hata kuwe na changamoto wanandoa wanatakiwa kuishi hadi kifo kiwatenganishe

Wanaume wa kiislamu pamoja na kuruhusiwa kuoa wake hadi wanne kutwa husingizia changamoto na kuoa wengine.

Mtu unaruhusiwa kuoa wake wanne huyo mmoja akikupa changamoto huwezu vumilia kidume wewe?

Akili huna za kuishi na mke kwa mujibu wa Biblia

Biblia inatamka wazi kuwa wanaume wanatakiwa kuishi na wanawake kwa akili..Na unapooa huwa unaulizwa kama una akili timamù.Lengo la swali ni kujua kama una akili za kuishi na mke. Ukiona mwanaume anampa talaka mkewe au anasema mke kanishinda ujue huyo mwanaume akili timamu hana za kuishi na mwanamke.Kifupi huyo mwanaume alitakiwa kuwa padri wa kanisa katoliki ambao hawao hawaoi.

Huyo mwanamke anayetaka kupewa talaka anatakiwa kumburuza mahakamani huyo mwaname huyu.mleta mada kwa kumtapeli na kumtaka amlipe fidia kubwa sana akielezea kuwa wakati anamuoa alijifanya kuwa ana akili timamu wakati kwenye ndoa kaonyesha wazi mambo mengi nyumbani na kwenye ndoa anaonyesha wazi akili hana.Na atoe ushahidi mfano hatunzi familia nk nk
 

Thread closed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…