Utaratibu wa Manispaa Kulipishwa Faini ya Kujenga Bila Kibali

ComputersDAR

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
213
Reaction score
242
Wakuu heshima kwenu

Nahitaji msaada kuhusu utaratibu wa Manispaa pale ambapo mhusika amegundulika kuwa ameanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya kawaida isiyo ghorofa kwenye kiwanja chake halali kisicho na mgogoro wowote lakini bila ya kuwa na kibali cha ujenzi kuoka manispaa.

Jee, ni sawa kama mtu ameanza ujenzi bila kibali na baadaye kwa hiyari yake kuamua kwenda manispaa na kuwasilisha maombi ya kibali cha ujenzi na hadi kulipia ada ya kibali, kulazimishwa kulipa fine ya 2% ya thamani ya jengo lake?

Au kuna sababu nyingine za msingi pamoja na hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa awali kabisa na manispaa kama kupewa notisi ya kusimamisha ujenzi na muda wa kuanza utaratibu wa maombi ya kibali cha ujenzi kabla ya uamuzi wa kutoza fine ya kujenga bila kibali ilhali hujakamatwa na ulienda mwenyewe manispaa kupeleka maombi ya kibali cha ujenzi?

Nawasilisha
 
Mnakuza Sana Vitu vidogo, mambo mengine Malizia na mwenyekiti wa mtaa mpe kiasi cha mboga wala siyo issue.

Mtaa upo chini ya mwenyekiti, hakuna mtu wa kutoka halmashauri kukufuata wewe, mtaa ndio unajuwa yanayoendelea mtaani.
 
Labda kama unajenga kwenye squarter huko,ila cku hz wanakuja na ile mirangi ya simamisha ujenzi.
 
Wakuu heshima kwenu

Nahitaji msaada kuhusu utaratibu wa Manispaa pale ambapo mhusika amegundulika kuwa ameanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya kawaida isiyo ghorofa kwenye kiwanja chake halali kisicho na mgogoro wowote lakini bila ya kuwa na kibali cha ujenzi kuoka manispaa.

Jee, ni sawa kama mtu ameanza ujenzi bila kibali na baadaye kwa hiyari yake kuamua kwenda manispaa na kuwasilisha maombi ya kibali cha ujenzi na hadi kulipia ada ya kibali, kulazimishwa kulipa fine ya 2% ya thamani ya jengo lake?

Au kuna sababu nyingine za msingi pamoja na hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa awali kabisa na manispaa kama kupewa notisi ya kusimamisha ujenzi na muda wa kuanza utaratibu wa maombi ya kibali cha ujenzi kabla ya uamuzi wa kutoza fine ya kujenga bila kibali ilhali hujakamatwa na ulienda mwenyewe manispaa kupeleka maombi ya kibali cha ujenzi?

Nawasilisha
Kwani kulikuwa na ulazima wa kuwaambia umeshaanz ujenzi?,inaonyesha we ni bushlawyer,sasa na wenzako wanatembelea humohumo mpaka uelewe.
 
Mnakuza Sana Vitu vidogo, mambo mengine Malizia na mwenyekiti wa mtaa mpe kiasi cha mboga wala siyo issue.

Mtaa upo chini ya mwenyekiti, hakuna mtu wa kutoka halmashauri kukufuata wewe, mtaa ndio unajuwa yanayoendelea mtaani.
Wewe ndiye unafaa kuwa rais wa nchi hii, ukiingia madarakani anza kuivunja Takukuru watu wamaliziane mitaani.
 
Kwani kulikuwa na ulazima wa kuwaambia umeshaanz ujenzi?,inaonyesha we ni bushlawyer,sasa na wenzako wanatembelea humohumo mpaka uelewe.
Wameangalia satellite image kwenye mfumo wao wakaona kiwanja kina mjengo
 
Hizi Municipal Bylaws wanazotumia Manispaa nimetafuta sana sijaona wameweka utaratibu/mwongozo wa kulipa faini ya 2%.
 
Wewe unacomplicated maisha, Bongo utapata tabu Sana.

Ingekuwa hivyo usingeona Filling station zinatowa kama uyoga kila siku Hadi kwenye makazi ya watu.

Kujenga filling station unahitajika kuwa na kibali cha Nemc.
 
Wewe uncomplicated maisha, Bongo utapata tabu Sana.

Ingekuwa hivyo usingeona Filling station zinatowa kama uyoga kila siku Hadi kwenye makazi ya watu.

Kujenga filling station unahitajika kuwa na kibali cha Nemc.
Naunga mkono hoja.
 
Mimi walikuja naona wakanusa wakapata hbr sizo kwa mafundi wakasepa haraka ujenzi ukaendelea sijaona mtu
 
Mm pia alikuja mwenyekiti na mjumbe. Nikatoa kiasi cha mboga wakasepa mpk leo cjawahi kuwaona na marangi rangi saiti kwngu.
Wapoze tu
 
Back
Top Bottom