Utaratibu wa mikataba ya ajira

Utaratibu wa mikataba ya ajira

Poluyakhtov

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2017
Posts
358
Reaction score
300
Habari za muda huu wana JF,

Naomba kwa wataalamu wa sheria hasa zile za mikataba ya ajira mnisaidie hili swali,Je,ni utaratibu wa kisheria mtu kufanyiwa probation mara mbili yaani miezi mitatu kwanza na akifaulu hapo anaingia awamu ya pili ya miezi sita au zaidi?

Shukrani.
 
Habari za muda huu wana JF,
Naomba kwa wataalamu wa sheria hasa zile za mikataba ya ajira mnisaidie hili swali,Je,ni utaratibu wa kisheria mtu kufanyiwa probation mara mbili yaani miezi mitatu kwanza na akifaulu hapo anaingia awamu ya pili ya miezi sita au zaidi?
Shukrani.
mikataba ya majaribio/probation kisheria za kazi inapswa kuwa ya kipindi kisichozidi miezi 12.
mwajiri anaweza kutoa mkataba wa majaribio kwa muda wa miezi mitatu,miwili au zaidi ila iwe ndani ya kipindi cha miezi 12.
1: na endapo kama alitoa mkataba wa majaribio wa miezi 3 na ikaisha ,huku mwajiriwa ambaye yupo katika probation hajaweza kuonyesha utendaji mzuri katika kazi mwajiri lazima amfahamishe mwajiriwa juu ya tatizo hilo na kama itabidi anaweza kuongeza muda wa kufanya kazi katika kipindi kingine tena cha majaribio baada ya kukubaliana na mwajiriwa,na muda utakao ongezeka lazima uwekwe wazi kwa pande zote mbili kabla ya kipindi kingine cha majaribio kuanza.(lengo la kuongeza kipindi cha majaribio ni kumpa mfanyakazi muda wa kuboreka zaidi katika utendaji wake wa kazi)
2: kama kulikuwa na makubaliano ya awali ya kuongezeka kwa kipindi cha majaribio basi baada ya successful accomplishment ya kipindi cha kwanza cha majaribio lazima kipindi cha pili cha majaribio kiwepo kutimiza makubaliano yenu ya awali.
Turudi kwenye swali lako la msingi:
mwajiri anaweza kuongeza muda wa majaribio kutoka miezi 3 na zaidi ila haipaswi kuzidi miezi 12,japo kuwa kitaalamu ikipitiliza miezi 12 na hujapewa barua ya uthibitisho kama mfanyakazi au mkataba wa ajira pia huwezi kuwa mfanyakazi bali utabaki kuwa probationer employee tu.
ongezeko lolote la muda wa majaribio ambao haukuwa na prior agreement kati yenu hauta tambulika kisheria,na pasipo mwajiri kukupa taarifa ya maandishi au mdomo juu ya kusudio husika na sababu la ongezeko la muda.
kama hivyo vyote havijafuatwa unaweza kufungua kesi CMA (mwajiriwa wa sekta binafsi) kwa sababu ya UNFAIR LABOUR PRACTICES.
Natumai utakuwa umepata mwanga kidogo.
 
Back
Top Bottom