JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kwa mujibu wa kifungu cha 68 na 69 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 69 na 70 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kituo cha kupigia kura kitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni
Itakapofika saa 10:00 jioni:
(i) Endapo kutakuwa na wapiga kura kwenye mstari muda huo, mlinzi wa kituo atasimama nyuma ya mpiga kura wa mwisho ili mpiga kura mwingine yeyote aliyechelewa asiweze kuja na kupanga foleni mara baada ya muda wa kufunga kituo kufika. Wapiga kura walio kwenye mstari waruhusiwe kupiga kura hadi watakapokamilisha upigaji kura
(ii) Wapiga kura watakaofika kwenye kituo cha kupigia kura baada ya saa kumi kamili (10:00) jioni watakuwa wamechelewa na hawataruhusiwa kupiga kura
Upvote
0