habari wanaJF,
Naomba kujua utaratibu wa mwalimu wa kike kahama kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kumfuata mme wake, maana kuna mtu ametuma maombi ya kuhama ila kaambiwa na afisa elimu wake eti mpaka apate mtu wa kubadilishana naye. Cheti chake cha ndoa anacho na ameambatanisha copy yake kwenye ile barua.
Naomba mwenye kujua taratibu zaidi anijuze!!!!
mh, kazi mbona ipo kama ndo hivyo!!! shukrani sana mkuu, ntalifanyia kazi hilo!!!katika waraka wa uhamisho kwa watumishi wa serkali unamtaka mtumishi akae ktk kituo chake cha kazi kwa miaka mitatu ndipo aombe uhamisho,,ila aweza kuomba kuhama endapo atapata mtumishi wa kuziba pengo ataloliacha hii itapelekea wilaya za pembezoni mwa nchi kutokua jukwaa la kutafutia ajira serikalini.Ndio maana huyo kaambiwa atafute wa kubadilishana nae,,