Utaratibu wa Polisi kumtaka mtuhumiwa kujisalimisha mwenyewe ni sahihi?

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Nauliza naomba kufahamishwa:

Hivi jeshi letu la polisi huwa halina utaratibu/kanuni rasmi ya namna kumkamata (Arrest) mtu au mtuhumiwa, au hata kumwita afike kituoni.

Jee huu mtindo wanatumia sasa hivi wa kumtaka mtuhumiwa ajisalimishe ni sahihi? Au kumtaka raia yoyote afike kituoni kusaidia polisi ni sahihi?

Ninavyojua, labda uelewa wangu mdogo, ni kwamba kuna utaratibu wa kutia mbaroni mtu kwamba lazima polisi awe na arrest warrant na mtuhumiwa anaambiwa kosa lake hapo hapo. Au kinakuwapo kitu kiitwacho summons kuitwa shaurini.

Inawezekana polisi wanakalia kuburuza buruza tu raia kwa sababu raia hawajui rights zao?
 
Actually, polisi wakiomba mtu afike (ajisalimishe) mwenyewe kituoni ni heshima kubwa sana kwa mtuhumiwa. Njia mbadala ni kuja nyumbani au kwenye starehe zako (pub) na karandinga lao. Wakifanya hivyo (na wakiwa na warrant) sheria inawataka wakutie pingu halafu wakutupie nyuma ya Defender pickup - kila mtu akuone.

Ni njia ipi ya ukamatwaji ungeipendelea?
 
Utaratibu mzuri ni ule unakwenda Polisi kulalamika umepigwa na jamaa unapewa kikaratasi cha RB eti ukamlete mtu alokufumua mpaka ukakimbilia polisi!
 
Back
Top Bottom