Utaratibu wa timu kuanzia round ya awali halafu zingine zinasubiri round ya pili ni wa hovyoo sana

Ubarikiwe mkuu, nami sikulijua hili, sasa nimeelewa
 
Mkuu nifafanulie vizuri hapo kwenye wanachama 12 wanaotoa timu mbili mbili
Je ni Kwanin wao walipewa feva hii? Lengo lilikuwa nin
Je nao idadi yao hubadilika badilika au ni wale wale kila msimu
 
unajua kuwa huko ulaya hizi hatua za awali zipo?
 
huko Ulaya ambako tunaiga kila kitu wanazo hizi round tena huko kuna rounds zaidi ya tatu, mkuu kila kitu ni process hata kombe la dunia hata Tanzania tunashiriki ila mwisho wa siku zinahitajika timu 32 tu kwa dunia nzima yenye nchi zaidi ya 200


Afrika kuna nchi 50+ kwa maana yako CAF wachukue timu moja tu kila nchi zitachezwa mechi ngapi kwa muda gani?? ndo maana ukawekwa utaratibu kama huo nyingi zitoke chache zibaki
 
Mkuu nifafanulie vizuri hapo kwenye wanachama 12 wanaotoa timu mbili mbili
Je ni Kwanin wao walipewa feva hii? Lengo lilikuwa nin
Je nao idadi yao hubadilika badilika au ni wale wale kila msimu
points, kadri unavyofika hatua za mbali ktk mashindano ndio unavyozidi kukusanya points za kufanya nchi yako ipeleke timu mbili
 
Mkuu nifafanulie vizuri hapo kwenye wanachama 12 wanaotoa timu mbili mbili
Je ni Kwanin wao walipewa feva hii? Lengo lilikuwa nin
Je nao idadi yao hubadilika badilika au ni wale wale kila msimu

Favour inatokana na kufanya vizuri kwa vilabu vyao katika mashindano ya CAF ngazi ya vilabu. Mfano halisi ni Tanzania ni miongoni mwa mwanachama wa CAF, tulikuwa tunapata nafasi ya timu moja tu klabu bingwa lakini baada ya Simba kufanya vizuri kwa misimu kadhaa Tanzania ikaingia kwenye top 12.

Hivyo kwenye ranking ya CAF zipo rank za aina mbili, kuna club ranking halafu kuna association ranking. Hii association ranking huchukua jumla ya point zilizokusanywa na vilabu katika nchi husika na ndio huchukua vilabu 12 bora, nafasi ya kuingiza timu nne (mbili klabu bingwa na mbili shirikisho) Kwa Tanzania ina jumla ya point 71 hizi point 71 zimepatikana kutoka kwa vilabu vitatu
1) Simba point 39
2) Yanga point 31
3) Namungo point 1
Hivyo hizo point 71 imeifanya Tanzania kuwa ya 6 kwenye association ranking ya CAF.
 
Nadhani CAF inatakiwa kufanya review katika baadhi ya mambo yake . Hii ni taswira ya kibaguzi. Pia na suala la timu kubwa kuanzia ugenini nao huu ni utaratibu wa hovyoo sana.
Jana nimeangalia za kina JKU, DISCIPLES, ORLANDO PIRATES, BUMAMURU, VITAL'O itajua mexhi za awali ni muhimu.

Lazima hizi mechi ziwepo ilo kutoa vibonde, zibaki timu ambazo ni serious pekee.

Timu kama Disciples vs Orlando pirates zilikuwa zinacheza ujinga kabisa.

Pyramids inacheza na upuuzi tu wa JKU, ujinga mtupu.

Unaona kabisa gap liliopo kati ya Yanga, Pyramids na hivi vitimu vya Zanzibar, Djbouti, Botwasana, Burunei
 
Hapa nimeelewa kwanini mwaka jana CAF walitumia top 10 hazikuanzia hatua ya awali. Na mwaka huu siyo top 10 tena ila wametumia top 5
 
Haaahaaa!!! Hakika JKU ni upuuzi mtupu
 
Mkuu umeeleza vizuri kwa faida ya wengi wasiofuatilia mpira(nje ya pitch). Kwa kuongezea tu watu waelewe kwamba mazingira ya africa ni tofauti sana na Ulaya kuanzia miundombinu inayohusiana na mpira direct kama vile viwanja na ile inayohusika indirect mfano usafiri, hotel nk. Hivyo basi hatuwezi kuwa sawa exactly kama wao. Mfano ni hii sheria ya goli la ugenini au ya fainali mbili kwa kwetu huku binafsi naona ni sawa kwani timu za ugenini kwa kuzingatia factor nilizozitolea mfano hapo juu hupata matokeo wa mbinde wanapokuwa away we fikiria tu timu kama Coast kwenda Angola tu au Congo hapo kwa ndege ya abiria(hii ni kwa timu zenye uwezo kiasi) inalazimika kwenda mpaka Ethiopia kwanza ndo waunganishe ndege ya Angola tofauti na ulaya kusafiri nchi moja hadi nyingine ni chap kwa haraka
 
Jibu ni rahisi sana nashangaa wewe umemzungusha mleta mada kiasi kile kwa takwimu ambazo hazihusiani na kinachoongelewa. Jibu rahisi na la moja kwa moja ni kwamba timu zinazidiana viwango (wakiangalia rekodi zao za miaka ya karibuni) na ndiyo zinazoamua nani aanze hatua ya awali, nk.

Ndiyo maana nikadhani unatania maana umetiririka vitu sivyo.
 
Reactions: Tui
Nondo zote hizi iwe ni Joke..? Be serious chap..πŸ˜†πŸ˜„πŸ˜ƒ
Hahahah

Maisha yanaenda kasi sana. Ni juzi tu na wewe ulikuwa vibonde kama hao. Heshimuni mpira jamani, unadhani hizo timu na zenyewe hazitaki kushinda?
 
Reactions: Tui
Hahahah


Maisha yanaenda kasi sana. Ni juzi tu na wewe ulikuwa vibonde kama hao. Heshimuni mpira jamani, unadhani hizo timu na zenyewe hazitaki kushinda?
Mimi sidharau kibonde.

Hata Azam apambane atoke kundi la vibonde. Imagine, Namungo ana point 01, wakati Azam ni SIFURI
 
Ndio maana nilikwambia hauna hoja, umeishia kusoma content tu ya mleta uzi. Mwenzio nimesoma heading na content vyote kwa pamoja ndipo nikatoa majibu kutoka hoja zake mbili. Moja ilikuwa kwenye heading ( timu kuanzia raundi ya pili) na ya pili ni hilo la kuanzia nyumbani au ugenini. Usitake kulazimisha kudharauriwa na kila mtu. Sasa rudi usome heading ya mleta uzi kisha njoo useme ni takwimu gani haihusiana na kinachoongelewa.
 

Yote hayo yanahusiana na ranking, wekea nukta hapo! Sijaelewa kwa nini ukaamua kumpoteza mleta mada kwa kuingiza masuala ya idadi ya nchi, yaani ukaamua kumuingiza chaka kabisa mkuu wa watu, ni huzuni kwa kweli. Yote hayo ili kukwepa ukweli kuwa kirank, kitakwimu na kihistoria Yanga bado upo chini ndiyo sababu mpaka sasa inaanzia huku na timu za Djibouti.
 
Wewe jamaa una matatizo gani? Hiyo post niliyoweka attachment nimejibu comment ya mdau ambaye sio hata mleta uzi (post namba 7 ya Abuu Kauthar )Yeye kaja na hoja zake zinginezo na ndizo nilizokuwa nimemjibu kwa post namba 14 na nikamjibu kwa kumpa reference. Mbona una wenge? Maana unatafuta jambo kwa hudi na uvumba. Endelea kutafuta maana nakuona unajiabisha kwa kuleta vihoja badala ya hoja.
 
Duuh! Alichopost huyo wa 7 ndiyo hicho hicho alichopost mleta mada, alikuwa tu anamuunga mkono.

Na wewe hapo juu umenijibu kuwa ulipost vile baada ya kusoma heading na content ya mleta mada, hapa unakuja kuruka. Kwani heading, post 1 na ya 7 vinatofautiana nini? Halafu unanishangaa mimi, basi tushangaane!
 
Reactions: Tui
Kwenye uzi wa mleta mada kuna sehemu yeyote kasema kuwa ni ushamba CAF kutumia ubora wa miaka 7 nyuma kupima timu kwa wakati wa sasa?
Kama hajasema huoni kama mdau kawasilisha hoja yake mpya ya kwamba CAF ipo kizamani kwa kufanya ranking ya miaka 7?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…