Utaratibu wa usafi wa Mazingira nao uwekwe kwenye Katiba?

Utaratibu wa usafi wa Mazingira nao uwekwe kwenye Katiba?

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Utaratibu wa usafi wa Mazingira nao uwekwe kwenye katiba?

Nimekuwa nikitatizika sana na usafi wa mitaa yetu. Hakuna jitihada zozote zinazoongelewa kuhusu usafi wa mazingira yetu.

Inasikitisha sana kwamba tupo na ngazi za uongozi kutoka kwenye mitaa lakini hakuna utashi wa kuhimiza watu kusafisha mazingira.

Mitaa yote Dar es salaam haisafishwi kila wakati inatoa harufu mbaya. Utakuta Mwenyekiti wa mtaa yupo hawezi hata kuhimiza vijana wakachimbua hiyo mitaro na kusafisha mazingira.

Mfano: Dodoma maeneo ya Airport sehemu ambayo inamkusanyiko mkubwa wa watu Chako ni Chako mitaro inatoa harufu mbaya miezi yote 12.

Sababu za kutokea kwa jambo hilo
Hakuna political will Hapa naongelea utashi wa kisiasa. Hakuna viongozi wenye utashi wa kisiasa maana hakuna mwongozo wa kuwaelekeza kuhamasisha watu kufanya usafi. Matokeo yake imekuwa ni tabia na watu wanaona hilo ni jambo la kawaida. Lazima kuwepo na miongozo kikatiba itakayoweka misingi ya usafi wa mazingira. Hii itasababisha viongozi wa kisiasa waweze kuhimiza usafi wa mazingira.

Viongozi wa serikali za mitaa hawana ToR. Wanafanya kazi kwa kijitolea

Viongozi wa mitaa hakuna maelezo wala guidance iliyopo kuhusu usafi wa mazingira. Kwahiyo kunakuwa na ombwe la kutekeleza majukumu.

Hakuna taasisi inayohusika na usafi wa mazingira bali kunataasisi inayohusika na udhibiti

Tunakuwa tunakibilia katika kudhiti badala ya kuwa na taasisi ya kutatua changamoto. Mfano: National Environment Management Council (NEMC) Wamekuwa ni wadhiti tu badala ya wao kuwa watatuzi wa changamoto.

Mgongano wa Taasisi kiutendaji
Hapa kuna taasisi utitiri zinazojihusisha na mazingira. Kunakuwa hakuna mmoja nayekuwa responsible na usafi wa mazingira.

Utatuzi
Lazima katiba mpya iweke misingi ya usafi wa mwili na mazingira kwa kila raia wa Tanzania.

Katiba iweke takwa kwa viongozi kuhimiza usafi wa mazingira.

Mwenye maelezo mengine namkaribisha.
 
[09:45, 28/06/2023] Mz: Mimi nadhani suala zima la usafi wa miji yetu, hususa majiji yetu inayokua kwa kasi kubwa, hilijapewa kipaumbele na serikali kuu kwa miradi mikubwa inayohitajika; wala na pia na halmashairi kwa yale yaliyo chini ya uwezo wao.

Nitoe mfano wa jiji la Dar. Mifereji yote ya maji taka na ya mvua, inaelekea baharini. Miundo mbinu yake mikuu karibu yote, hasa kutoka katikati ya Jiji la Dar, ni ile ilyojengwa kabla ya Uhuru. Wakati huo Dar ikiwa na idadi ya watu kama laki tatu kama nipo sahihi. Tunategemea nini kwa hali kama hiyo!! Hili si swala la Katiba kwa maoni yangu. Bali ni ukosefu wa dhamira thabiti katika mipango ya usafi na utunzajj wa mazingira ya majiji na miji yetu.

Hivi jiji la Dar, linashindwa vipi kugawa hata mapipa ya taka kila nyumba, tena kwa kulipiwa na wenye nyumba?

Kweli wameshindwa kuweka utaratibu wa uhakika wa kuzoa taka aidha na halmashauri zenyewe au sekta binafsi bila bughudha kwa wazoa taka kupita kila mlango kudai malipo ya kusomba taka! Kwa mtindo huu wa sasa, unaondokanaje na usombaji wa taka kwa kutumia magari mabovu ambayo yenyewe ni taka pia, tena nyakati za msongamano wa magari barabarani!! Naamini baadhi ya watendaji wa majiji na miji yetu wamo kwenye group hii. Chukueni hatua.
 
[10:37, 28/06/2023] T: Ni kweli kuwa usafi wa mazingira ni suala muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na kusimamiwa kikamilifu. Kuweka utaratibu wa usafi wa mazingira kwenye katiba inaweza kuwa njia moja ya kuhakikisha kuwa suala hili linapewa umuhimu na kutekelezwa kwa ufanisi. Nina machache kuhusu umuhimu wa kuweka utaratibu huu kwenye katiba:

Kuongeza umuhimu wa usafi wa mazingira: Kuweka utaratibu wa usafi wa mazingira kwenye katiba kunathibitisha umuhimu wa suala hili kwa jamii na serikali. Inafanya usafi wa mazingira kuwa haki ya kimsingi ya kila raia na inahimiza wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua za kuhifadhi mazingira safi.

Kutoa mwongozo wa kisiasa: Katiba yenye miongozo ya usafi wa mazingira itasaidia kuunda mwongozo wa kisiasa na kuweka wajibu kwa viongozi wa serikali na taasisi za mitaa kuhusu jukumu lao katika kuhamasisha na kusimamia usafi wa mazingira. Itasaidia kujenga utashi wa kisiasa na kukuza uwajibikaji wa viongozi.

Kuwezesha utengenezaji wa sheria na sera: Utaratibu wa usafi wa mazingira kwenye katiba unaweza kuwa msingi wa kutengenezwa kwa sheria na sera madhubuti za kusimamia usafi wa mazingira. Sheria na sera zilizoimarishwa zitatoa mwongozo wazi na taratibu za kutekeleza usafi wa mazingira na kuweka adhabu kwa wale wanaovunja sheria hizo.

Kuunda taasisi na miundo ya usimamizi: Katiba inaweza kutoa miongozo ya kuanzisha taasisi na miundo ya usimamizi wa usafi wa mazingira. Hii itasaidia kuondoa mgongano wa majukumu na kuweka taasisi husika inayowajibika kwa usafi wa mazingira. Taasisi hizo zinaweza kuwa na mamlaka ya kusimamia, kutoa mafunzo, na kutekeleza mikakati ya usafi wa mazingira.

Kuhamasisha umma: Katiba yenye utaratibu wa usafi wa mazingira inaweza kuwa chombo cha kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa suala hili. Inaweza kutoa jukwaa la kielimu na kukuza uelewa wa umma juu ya athari za uchafuzi wa mazingira na umuhimu wa kuchukua hatua za kuzuia na kutunza mazingira yetu.

Ni muhimu kutambua kuwa kuweka utaratibu wa usafi wa mazingira kwenye katiba ni hatua ya kuanza. Baada ya kuweka misingi hiyo, itakuwa muhimu kutekeleza sheria, sera, na mipango ya vitendo ili kuhakikisha kuwa usafi wa mazingira unafanyika kikamilifu na kudumu. Pia, ushirikiano kati ya serikali, taasisi za mitaa, na jamii nzima utakuwa muhimu katika kufanikisha lengo la usafi wa mazingira. Na uzuri Tuna viongozi na wataalamu wa NEMC hapa watatuongoza katika mjadala huu uliouleta
 
Ni muhimu kutambua kuwa kuweka utaratibu wa usafi wa mazingira kwenye katiba ni hatua ya kuanza. Baada ya kuweka misingi hiyo, itakuwa muhimu kutekeleza sheria, sera, na mipango ya vitendo ili kuhakikisha kuwa usafi wa mazingira unafanyika kikamilifu na kudumu. Pia, ushirikiano kati ya serikali, taasisi za mitaa, na jamii nzima utakuwa muhimu katika kufanikisha lengo la usafi wa mazingira. Na uzuri Tuna viongozi na wataalamu wa NEMC hapa watatuongoza katika mjadala huu uliouleta
 
Jambo la kuanzia nalo ni kutunga sheria ngumu na nzito kulinda misitu yetu na vyanzo vya maji.
Hili suala la usafi litakuja automatically.
 
Back
Top Bottom