Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Halmashauri ya Jiji hawa watu wenu wa Suma JKT wamefeli hili zoezi la kuzoa taka maana inavyoonekana Wanamagari machache, hivyo kusababisha kushindwa kupita karibia kila mtaa kwa wakati.
Ukipita mitaa ya Mwanjelwa, Soweto, Mwambene, Kabwe, Isanga, Uyole na mingine mingi utaona namna taka zilivyotapakaa mitaani.
Pamoja na hivyo, ukipita kwenye yale maeneo wanayoishi viongozi kila siku gari zinakwenda na kuzoa taka lakini huku kwetu Wakina ‘Uswazi’ gari linapita kwa wiki mara moja au mara mbili.
Mbaya zaidi wananchi wanaamua kwenda kuzirundika taka hizo pembezoni mwa Barabara na wengine wanazitupa kwenye mitaro ya maji.
Licha ya gari kusumbua kubeba taka hizo lakini wale ndugu zetu wa kukusanya fedha za taka wao kila mwezi lazima wafike na kudai fedha.
Utaratibu wa fedha ya taka ni kila mlango ni Shilingi 2,000, yaani kama nyumba moja ina wapangaji saba, basi kila mpangaji anatakiwa kutoa kiasi hicho.
Kwa wafanyabiashara wa maduka, wao wanatakiwa kutoa shilingi 5,000 kila mwezi, Lodge yenye bar na restaurant inatakiwa kulipa kiasi cha Shilingi 20,000/=, Lodge peke yake inalipa kiasi cha Shilingi 10,000/=.
Inafika kipindi huwa najiuliza ni vigezo gani walitumia mpaka waliamua kuipa Mbeya hadhi ya kuwa Jiji kama vitu vidogo tu hivi vya kukusanya taka vinawashinda.
Hali ni mbaya sana maeneo ya Kabwe Stand maana kuna takataka zinarundikwa pale na maeneo ya karibu na biashara za vyakula zinaendelea.
Nakumbusha Mamlaka zinazohusika zisiishie kuwafungia hao Mama Lishe na Baba Lishe pamoja na hivyo visima vya maji, bali maadamu mnakusanya pesa zetu za taka basi kumbukeni kuzoa hizo taka.
Pia soma:
~ Mbeya: Wazazi tutoe elimu ya chakula kwa Watoto wetu kuanzia nyumbani ili iwe tahadhari ya kujilinda na Kipindipindu
~ Wagonjwa wa Kipindupindu wafikia 22 Mbeya, na Serikali imepiga kimya!