BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Katika hali inayoonyesha vita vya kampuni za uwindaji nchini, Serikali imeingia katika lawama ya upotevu wa mapato na kuzisababishia hasara kampuni sita zilizoshinda zabuni ya uwindaji kwa wenyeji na wageni wakazi iliyoendeshwa Agosti, 2021.
Taarifa ilizozipata Mwananchi zinaonyesha kampuni zilizoshinda zabuni hiyo ni pamoja na A Class Hunting and Safari Limited iliyoshinda katika kitalu cha Talamai (Manyara), Nundu Hunting Safari iliyoshinda kitalu cha Kisarawe (Pwani), Monster Daggaboy hunting Ltd iliyoshinda kitalu cha Simbanguru Igwamadete (Singida).
Nyingine ni Mbogo Wild Meat Butcher iliyoshinda kitalu cha Matundu Forest (Morogoro), Suleiman Masoud Suleiman aliyeshinda katika kitalu cha Kilwa (Lindi) na kampuni ya Jungle Butcher iliyoshinda kitalu cha Ipemba Mpezi (Tabora).
Hata hivyo, licha ya kampuni hizo kushinda na kulipia ada ya Sh282.50 milioni, hazikupewa zabuni hiyo baada ya kampuni ya Tachaco Hunting Safari Group Ltd – (TACHA) kulalamika kuwa mnada huo uliingiliwa, kudukuliwa na kwamba haukuwa wazi wala huru.
Akizungumza na Mwananchi kwa niaba ya kampuni hizo, Murugenzi Mkuu wa A Class Hunting and Safaris Limited, Japhari Mohamed alimtaja aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro (sasa Waziri wa Katiba na Sheria) kuwa ndiye aliyesimamisha mnada huo kinyume na utaratibu.
“Tulifuata taratibu zote ikiwa pamoja na kulipa ada zinazotakiwa, lakini tunashangaa waziri alisitisha mnada, kwa madai kuwa umeingiliwa,” alisema Mohamed katika mahojiano na gazeti hili.
Aliendelea kusema kuwa kampuni hizo zimelipa ada za mwaka mara tu mnada ulipokwisha Agosti 22, 2021 na kuongeza mapato katika ukusanyaji kodi.
Alisema endapo zabuni hizo zingeruhusiwa, Serikali ingepata mapato ya zaidi ya Sh1.23 bilioni ikiwa ni mapato ya uuzaji wa nyara kutoka kwa wawindaji wenyeji na wageni.
Kwa hatua hiyo, alisema ajira 120 zikiwemo 72 zisizo rasmi zimepotea. Hata hivyo, akizungumzia malalamiko hayo Mwenyekiti wa Chama cha Uhifadhi na Uwindaji (Tacha), Kanali Mstaafu Thomas Ndonde alisema mnada huo haukuwa ukitenda haki.
“Yaani kwa mfano kwenye zabuni tunaomba pori la Katavi, lakini kwenye teknolojia linatokea pori la Kilwa, sasa unachanganyikiwa kwamba mbona tulikuwa tunaomba pori Kilwa, limetokea pori la Katavi? Wakasema hiyo ni computer error (makosa ya kompyuta), alisema.
Aliendelea kusema, pori walilokuwa wamelikusudia kwa bei ya sh. 10 milioni, likafika sh. 103 milioni na kuongeza “tukaona hatuwezi kuligharimia, hata tukiwinda mwaka mzima, kwanza tukajiuliza tutarudishaje mapato ya serikali kila mwaka?"
Baada ya mnada huo kupita na kampuni zilizoshinda kutajwa, alisema walikwenda kulalamika kwa Waziri (wakati huo Dk Ndumbaro), ambaye naye aliziita pande mbili kusikiliza malalamiko.
Alisema miongoni mwa malalamiko yao ni kuona baadhi ya kampuni zikibandika matangazo ya uwindaji wa kitalii kwenye mapori waliyoshinda, ilihali zanbuni iliyotangazwa ni ya uwindaji kwa wenyeji.
“Hatimaye mwezi uliopita (Julai), wakatuletea taarifa kwamba tumetengeneza kanuni mpya, hebu njooni Arusha mzipitie, ndipo tukaenda,” alisema. Alisema kinachosubiriwa ni kuzisaini kanuni hizo na hatimaye kuanza kazi hiyo.
Mwananchi lilimpomtafuta Waziri Ndumbaro kwa simu alisema suala hilo iiulizwe Wizara ya Maliasili na Utalii.
“Nenda huko Maliasili watakupa taarifa, kwa sababu Maliasili ni wizara siyo mtu, kwa hiyo nenda Maliasili watakupa taarifa, kama una swali na Katiba na Sheria karibu,” alisema na kukata simu yake.
Alipotafutwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana alimtaka mwandishi kumtafuta Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Eliamani Sedoyeka, ambaye alikiri kuwepo ucheleweshwaji wa suala hilo na kuwa tayari kampuni hizo zimeshajulishwa.
“Walishaambiwa kwamba kulikuwa na irregularities (kasoro) nyingi kwa hiyo waziri alisitisha ile process (mchakato) nzima kwa kuwa haukuwa sawa na hata ukirudiwa hautakuwa sawa,” alisema.
Profesa Sedoyeka alisema pia mabadiliko hayo pamoja na yale ya mawaziri yamesababisha kucheleweshwa zaidi kwa suala hilo.
“Kiuhalisia malalamiko yao ni ya msingi, lakini sasa kulikuwa na mabadiliko ya mawaziri na makatibu wakuu, kwa hiyo suala lao linaenda linasimama, kwa hiyo mimi ndiyo naharakisha ili tumalize,” aliosema.
Alitahadharisha kuwa suala hilo ni nyeti kwani likiharakishwa linaweza kufikishwa mahakamani.
Kuhusu fedha zilizolipwa na kampuni hizo alisema, “ni kweli zile fedha walizolipa itabidi warudishiwe na ndiyo kitu nilichokuwa nakifuatilia.”
Akifafanua zaidi, Profesa Sedoyeka alisema awali, wazabuni walikuwa wanapewa zabuni kwa majadiliano hali iliyokuwa inachochea rushwa lakini mfumo wa mnada wa kielektroniki nao umekuwa na changamoto.
“Electronic ilipofanyika ikaonekana ina shida nyingi zaidi, kuna watu wanachezea mifumo, kwa hiyo waziri akasema hapana. Lengo lilikuwa zuri lakini matokeo yalipotoka yameleta malalamiko zaidi, ndiyo sababu waziri alisema turudie upya,” alisema.
Hata hivyo, alisema hata wangerudia, wasingepata matokeo mazuri lakini wameshakutana na wadau na kupitia upya kanuni.
Alipolizwa kuhusu ufanyaji kazi wa mfumo huo hadi uingiliwe, Profesa Sedoyeka alisema “kilichotokea nadhani ni upya wa mfumo ndio ikaonekana uangaliwe, inawezekana kulikuwa na presha, labda haukuwa na ukamilifu.
“Wale walioshinda wanasema hata kama ni tatizo la mfumo ni la kwenu, lakini na walioshindwa wanalalamika na ukifuatilia unaona yote yana tija,” alisema.
MWANANCHI