MasterGamaliel
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 923
- 1,001
Hivi huwa mnaogopa nini kutandika makofi wahalifu?Salam,
Kumekuwa na hii ya askari wa usalama barabarani kusimamisha gari kwa ajili ya ukaguzi na kumvizia driver akiwa hajazima gari na kuchomoa ufunguo wa gari ya aina ya Mitsubishi hasa Canter na Fuso, ikiwa ufunguo utachomoka wanakukamatisha kuwa ignition switch mbovu hivyo wanataka uandikiwe receipt ya ujuzi wao kwa TAS 30,000/= , sasa je kwa utalaamu ni kweli Mitsubishi canter na Fuso wana tatizo hilo au kwao Japan sio kosa. Na je kwa Tanzania ni kosa? Je kama tatizo linajirudia kwa magari mengi ya aina hiyo ni issue ya kunyamazia kwa Askari wa usalama barabarani au wanapaswa kureport kuwa this is unusual na kwamba kama nchi tujue cha kuamua kitija?
Wanawadekeza wenyewe hao traffic, mimi hata leseni yangu sasa hivi siwapi labda waniulize maofisa wa TRA.Hivi ethically Polisi anaruhusiwa kuizima gari iliyopo kwenye muungurumo?
Hivi ethically Polisi anaruhusiwa kuizima gari iliyopo kwenye muungurumo?
Nasikia mamlaka ya mapato imeshindwa kukusanya kwa kuwa biashara zimedorora, kazi ya kukusanya wameachiwa yangeyangeWanajichanganya kaka, Trafic wapo na majukumu tofauti tofauti sana, lakini kwa sasa wote wanafanya kazi zinazofanana, trafic mwenye ruhusa ya kufanya ukaguzi wa gari ni yule mara zote huwa na koti (Vehicle Inspector), hawa wengine hawana hiyo sifa ya kufanya ukaguzi kwenye gari, kazi yao ni kuangalia SHERIA ZA BARABARANI ZINAFUATWA kikamilifu
Shida iko hapa. Unaweza kukuta basi la Abiria lina tairi mbovu, so Hatari ya kuwa na tairi mbovu ni kuwa unaweza kupasuka wakati wowote na kusababisha ajali yenye kusababisha upotevu wa maisha, cha ajabu badala ya kulisimamisha gari na kumshurutisha mwenye gari kufunga tairi salama, wao wanakutoza faini na kukuachia uende, sasa maana iko wapi?