Utata kwenye nyumba tuliyopanga

Utata kwenye nyumba tuliyopanga

FK21

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2019
Posts
8,600
Reaction score
10,760
kama kichwa cha habari kinavyo jieleza ndugu zangu kuna mpangaji
mwenzangu naona kabisa sio mtu mzuri kwanza anazungumza sana kuhusu uganga na mambo ya kuogofya kwenye simu tena kwa kupayuka kingene pindi ana hamia alikuja na
vidada viwili miaka 17 na 18 tukajua ni nduguze ila sio nduguze kumbe sio tuligundua baada ya mmoja kumtaka wale madada wakaondoka juzi kaleta wengine age iyo iyo
wakati najiandaa kwenda kazini nikaitwa na hao wanaokaa nae chumba kimoja hao wabinti kwa dirishani kaka njoo utufungulie kwenda kawafungia kufuli nje je hiyo ni sawa
 
Ngoja tukusaidie kuandika vizuri, sio hadi Mods:

Tatizo la Mpangaji Mwenye Tabia Zisizofaa

Ndugu zangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kuna mpangaji mwenzangu ambaye kwa kweli si mtu mzuri. Kwanza, anazungumza sana kuhusu uganga na mambo ya kuogofya kwenye simu, tena kwa kupayuka. Pindi alipohamia, alikuja na wasichana wawili wa miaka 17 na 18. Tulidhani ni ndugu zake, ila tuligundua baadaye kuwa si ndugu zake, hasa baada ya mmoja wa wasichana hao kumtaka.

Wasichana hao waliamua kuondoka, na juzi mpangaji huyu kaleta wasichana wengine wa umri ule ule. Asubuhi moja, wakati najiandaa kwenda kazini, nilitwa na wale wanaokaa naye chumba kimoja. Wasichana hao waliniita kwa dirishani wakisema, "Kaka njoo utufungulie." Ilibainika kuwa mpangaji alikuwa amewafungia nje kwa kufuli.

Swali langu ni je, kitendo hiki ni sawa? Hali hii imetufanya tuwe na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama na ustawi wa wasichana hao na hali ya mpangaji huyo. Ni muhimu kuchukua hatua ili kuhakikisha usalama wa wote na kuhakikisha tabia zisizofaa hazifanyiki kwenye makazi yetu.
 
Punguza haraka na uandike vizuri
 
Hongera Kwa kuandika upya
 
Toa taarifa kwa kitongoji yeye atafata polis kufatilia kama ni swalama au kuna mambo ambayo ni kinyume na sheria hasa kama anawateka
 
Mambo ya watu wachie wenyewe ,akikugeuzia kibao utaanza oo wanadam sio watu,umesahau kuwa na wewe sio mtu maana yeye hakutaka kujua unaishije chumbani kwako ,kikubwa mtonye mwenye nyumba then yeye auone uongozi,,kosa kubwa ulilolifanya kufungua chumba cha mtu bila uongozi akikuambia milions zimepotea na akakana hapakuwa na mtu humo ndani Bali umefungua chumba kumwibia,huruma itakuponza.
 
Ngoja tukusaidie kuandika vizuri, sio hadi Mods:

Tatizo la Mpangaji Mwenye Tabia Zisizofaa

Ndugu zangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kuna mpangaji mwenzangu ambaye kwa kweli si mtu mzuri. Kwanza, anazungumza sana kuhusu uganga na mambo ya kuogofya kwenye simu, tena kwa kupayuka. Pindi alipohamia, alikuja na wasichana wawili wa miaka 17 na 18. Tulidhani ni ndugu zake, ila tuligundua baadaye kuwa si ndugu zake, hasa baada ya mmoja wa wasichana hao kumtaka.

Wasichana hao waliamua kuondoka, na juzi mpangaji huyu kaleta wasichana wengine wa umri ule ule. Asubuhi moja, wakati najiandaa kwenda kazini, nilitwa na wale wanaokaa naye chumba kimoja. Wasichana hao waliniita kwa dirishani wakisema, "Kaka njoo utufungulie." Ilibainika kuwa mpangaji alikuwa amewafungia nje kwa kufuli.

Swali langu ni je, kitendo hiki ni sawa? Hali hii imetufanya tuwe na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama na ustawi wa wasichana hao na hali ya mpangaji huyo. Ni muhimu kuchukua hatua ili kuhakikisha usalama wa wote na kuhakikisha tabia zisizofaa hazifanyiki kwenye makazi yetu.
Hapa nimeelewa,sasa jibu sio sawa mripotini kwa mjumbe ili ijulikane kwanini anawafungia hao mabinti
 
Labda ni mganga,hao mabinti ni wateja wake anasubiri Giza liingie awapakaze dawa.
 
Huwa sina muda na wapangaji washirikina,ila cha msingi asiingie anga zangu,watu tumekaa na mdada mpangaji anaongea kwenye mlango wa kutokea nje,ikifika saa 6 usiku anatoka kuoga,sasa asubuhi pananuka mikojo na sisi tunapotoka tunakanyaga hapohapo alipokuwa anaogea,mwingine alikuwa anamwaga mafuta chooni yalikuwa yanatoa harufu mbaya,na hiyo harufu ukisimama dirishani kwake unasikia.Lakini tulikomaa hadi walihama wenyewe
 
kaka mjini apa wewe maindi life lako tu achana na mganga na wateja wake., sijawahi kuona mganga anateka watu hao ni watu wazima na wamejipeleka wenyewe. so wewe fumba macho
 
kama kichwa cha habari kinavyo jieleza ndugu zangu kuna mpangaji
mwenzangu naona kabisa sio mtu mzuri kwanza anazungumza sana kuhusu uganga na mambo ya kuogofya kwenye simu tena kwa kupayuka kingene pindi ana hamia alikuja na
vidada viwili miaka 17 na 18 tukajua ni nduguze ila sio nduguze kumbe sio tuligundua baada ya mmoja kumtaka wale madada wakaondoka juzi kaleta wengine age iyo iyo
wakati najiandaa kwenda kazini nikaitwa na hao wanaokaa nae chumba kimoja hao wabinti kwa dirishani kaka njoo utufungulie kwenda kawafungia kufuli nje je hiyo ni sawa
Kamshitaki polisi, huyo jamaa ni Mpemba au, nimeuliza hiyo maana wao ni washamba wa kufuga wake zao ndani wasijuane hata na majirani.
 
Back
Top Bottom