moonlightj12
Member
- Dec 6, 2022
- 33
- 90
Wasalam wakuu, nimepata changamoto kidogo kwenye hii taasisi
Mzee wangu anasumbuliwa na Cancer alifanyiwa operation wakatoa uvimbe, then tukapewa referral kwenda Ocean Road Cancer Institute tulipofika tulipokelewa tukapewa utaratibu.
Tukaambiwa tulipie shilingi milioni tatu na laki sita kwa ajili ya dawa ambayo Mzee anatakiwa apewe, tukiwa tunajikanyaga tufanyaje kuna Mzee tulikuwa naye akatueleza kuna msamaha.
Tukafuatilia huo msamaha tukalipia shilingi milioni moja na laki sita, tukapewa maelekezo ya vyakula Mzee ambavyo hatakiwi kula na muda ambao tunatakiwa kurudi hospitali hapo.
Stori linaanza hapa, sasa tarehe ya kurudi Mzee imefika hawapigi simu, ikabidi tujichange tutafute nauli aende hukohuko Jijini Dar es Salaam.
Jamani unaweza lia basi tu hawa watu hawajui utafutaji wetu ulivyo wa shida, wanamwambia Mzee tulifanya mistake mara tuli-misplace risiti, mara kuna deni kubwa South Africa vitu ambavo personally nimeshindwa kuvielewa.
Hilo ni tisa, kumi wamemwambia kuna watu mbele yake ambao wameshaagiziwa hizo dawa, kwa hiyo yeye asubiri tena miezi miwili mbele, watampigia simu.
Kuna vyakula alikatazwa saizi wamemruhusu eti hadi watakapomgia simu watamwelekeza tena na upya.
Nyie watu mlioko huko maisha yetu ni magumu sana na hiyo hela mliipa 'limitations' ilipwe kwa wakati lakini saivi mnatuzungusha Mzee wangu anatoka mbali hadi kufika Dar anachoka sana.
Mungu anawaona lakini...
=============
Updates...
Dkt. Tausi Maftah
UFAFANUZI KUTOKA HOSPITALI YA OCEAN ROAD
Daktari Bingwa wa Mionzi ya Nyuklia, Dkt. Tausi Maftah wa Ocean Road anafafanua kuhusu malalamiko ya Mdau huyo:
Nianze kwa kueleza historia kwa ufupi, matibabu ya mionzi ya Nuklia huwa yanategemea na aina ya Saratani ya mgonjwa.
Msambazaji mkubwa wa dawa zetu za Mionzi ya Nyuklia yupo Afrika Kusini, mwingine ambaye tunamtumia kama akiba pale inapobidi yuko Ulaya.
Tunapofanya kazi na Msambazaji wetu wa Afrika Kusini ni rahisi kwa kuwa tunawasiliana naye kwa ukaribu na hata inapotokea kuna mabadiliko ya ‘oda’ za dawa ni rahisi kufanya maadiliko tofauti na yule wa Ulaya.
Pia itambulike kuwa Dawa tunazoagiza kutoka Afrika Kusini zina gharama kubwa na Serikali inachangia kwa asilimia kubwa kuwezesha zinafika Tanzania.
Mbali na hapo dawa zinazoagizwa kwa ajili ya Wagonjwa wa Saratani kutoka Afrika Kusini huwa zinakuja kwa oda maalum, mbali na hapo kitaalam dawa hizo huwa zina muda wake maalum (time limit), muda ukizidi hapo inaharibika na haziwezi kufaa kwa matumizi.
Hivyo, ni jambo gumu kuweka oda kisha ije na umpatie mgonjwa mwingine au usimpe mhusika, haiwezekani kuiweka tu.
Hata huyo Mdau aliyelalamika ni wazi anajua taratibu zote zinazofanyika ndio maana kaelezea kwenye maelezi yake, labda inawezekana hakuwa na subira ya kusubiri dawa, changamoto kama hiyo huwa inatokea mara kadhaaa kwa baadhi ya Wagonjwa kushindwa kuwa na subira wakati wa kusubiri dawa.
Aidha, kabla ya Dawa kutufikia (Tanzania) huwa zinatengenezwa kulingana na oda za wenye uhitaji, hatuwezi kuagiza dawa ambazo hazipo kwenye oda kwa kuwa zitakuja na kuharibika huku.
Hapo kati zikishatoka Afrika Kusini kunakuwa na michakato mingine kadhaa ikiwemo ukaguzi wa TMDA.
Hata wao TMDA waliwahi kutushauri tuagize dawa za miezi sita tukawajulisha hilo haliwezekani kwa kuwa dawa zinaagizwa kwa od ana zinakuja kwa wagonjwa maalum, pia time limit inatubana.
Tunachokifanya wakati mgonjwa anapokuwa anasubiri oda ya dawa zake kwenye mifumo yetu kunakuwa na maelekezo yote muhumu kuhusu yeye na anajulishwa kabisa kuwa Dawa yake inatarajiwa kufika lini, anapangiwa ratiba yake ya matumizi ya chakula na taratibu nyingine.
Uagizaji wa Dawa unaweza kuchukua wiki mbili hadi mwezi, huwa inategemea na oda ya dawa zilizoagizwa.
Wagonjwa wetu sisi ni rafiki zetu kwa kuwa huduma wanayopata hapa si ile ya kundikiwa dawa na kutakiwa kwenda, bali wanapewa maelekezo na tunawapa muda wa kuwasikiliza.
Kuna dawati la malalamiko na wapo huru kutoa malalamiko yao, wapo huru, hivyo changamoto zipo lakini ni suala la kueleweshana tu.