Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,894
- 76,810
Historia Inaonyesha Wanyamlenge/ wanyarwanda wameishi Mashariki mwa DRC kuanzia karne ya 19. Wengi walipelekwa na serikali ya kibelgiji na baadae wengi walihamia miaka ya 60-65.
1971 serikali ya Mobutu iliwapa uraia japo wananchi wengi wa Congo walilipinga hili. Hii tension ilisababishwa na wao kushiriki katika operation Simba. Iliyomtoa Lumumba madarakani.
Kitendo cha wananchi kukataa baadhi ya watutsi kupewa uraia kilisababisha iwe political agenda ya wanasiasa wa Kivu...baadhi ya watutsi walivuka mipaka kuiunga mkono RPF(kikundi cha watutsi kilichofanikiwa kuitoa serikali ya kihutu madarakani) chini ya Kagame.
Mauaji ya 1990s ya Burundi na Rwanda yalipelekea wakimbizi wa Kihutu kukimbilia Congo walipo Wanyamlenge (tutsi wa Congo) tayari hii ni tension.
Hawa wahutu waliunda vikundi kulipiza kisasi kwa Watutsi...moja ya kundi mashuhuri ni FDLR.
Kumbuka Mobutu aliiunga mkono serikali ya kihutu Rwanda. Miaka hiyo hiyo Laurent Kabila anasaidiana na Rwanda na Uganda chini ya ADFLC anaingia Congo kupitia mashariki walipo M23 na anafanikiwa kuichukua nchi.
Laurent Kabila akabadili jina la Zaire na kuwa DRC kama ilivyokuwa awali. Tension ikaongezeka kati ya watutsi wa Congo na wahutu(kumbuka pia Congo kuna wahutu asilia) waliohamia kukimbia mauaji ya kimbari.
Kagame na Museven walipoingia Congo kipindi cha kumsaidia Kabila hawakutoka ...lengo likiwa wavimalize vikundi vyote vya kihutu vinavyoitishia Rwanda. Hili lilileta taharuki saana....wacongo waliunda vikundi vya kujikinga na jeshi la Rwanda...mwaka 1998 kama sijakosea yakatokea mauaji ya wakongo zaidi ya 1000...Kasika massacre.
Kabila anayafukuza majeshi ya Rwanda na Uganda. Rwanda ilikataa kwendaa wakaanzisha vikundi kama RCD kutetea maslahi ya Watutsi.
Mwaka 2001 Kabila anauliwa , Kabila JR anachukua nchi.... Kabila Jr alifanikiwa kukaa chini na vikundi vya waasi akiwemo Laurent Nkunda na CNDP makubaliano yakiwa viwe vyama vya kisiasa na vijana waingizwe ndani ya jeshi.
Mwaka 2004 Laurent Nkunda akaungana na RCP kuwalinda Banyamlenge baada ya kulalamika kutokuridhika na serikali ya Kabila.
Mwaka 2009 March 23, waka kaa tena na serikali ya Kabila Jr. Baada ya kukamatwa kwa Nkunda na CNDP ikawa Chama cha siasa na waasi wakaingizwa jeshini. Wananchi wengi hawakupendezwa na hili. Likawa tena suala la kisiasa ...wanasiasa wakalitumia....mwaka 2012 vita ikaanza tena....kwa jina la M23
2013 zaidi ya nchi 10 za Africa zikasaini mkataba wa amani waasi wakakimbilia Uganda.
Mwaka 2021 wakarudi na kiongozi mwingine mpya...chokochoko zikaanza....Tshekedi akakimbilia EAC...baadae akawafukuza walinda amani wa EAC akaenda SADC.....
Tshekedi ni kabila moja na Laurent Kabila. Kabila Jr vyanzo vingi vinadai mama ni mtutsi na huenda sio mtoto halisi wa Kabila Sr.
Mgogoro unahistoria kubwa saana.....