elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,733
Ikiwa yapata zaidi ya miaka 40 toka auawe aliyekuwa raisi wa Marekani JF Kennedy, kifo chake kimegubikwa na utata mwingi na ukweli wa waliohusika na tukio hilo la kuawawa kwake si ajabu mpaka leo hawajawahi kuwekwa wazi.
Japo japo Lee Harvey Oswald alikamatwa na kushitakiwa kwa mauaji ya Kennedy ambapo alituhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji hayo akiwa peke yake bila kumshirikisha mtu jambo ambalo lilileta utata baina ya wapelelezi wenyewe wakipingana kuhusiano na jambo hili ya kwamba Oswald alipanga na kutekeleza mpango huo akiwa peke yake.
Jambo lingine la kustajabisha ni mfululizo wa mauaji au vifo vilivyo jitokeza na hitimisho lake kusemekana kwamba wahanga wajiua wenyewe, na watu hao walikuwa na fununu au walikuwa mashuhuda katika tukio la kuawa raisi JF Kennedy.
Baadhi ya watu/mashahidi waliouawa ni kama wafuatao.
Jack Ruby:
Huyu alimuua Oswald mbele ya wana habari katika tukio lililokuwa linarushwa moja kwa moja kwenye TV. Alimuua Oswald siku ya pili baada ya Oswald kukamatwa akituhumiwa kwa mauaji ya Kennedy, Ruby alimuua Oswald kwa kumpiga risasi ya kichwa mbele ya wanahabari.
Jambo la kustaajabisha ni kuwa, Ruby alikuwa umbali wa mita kadhaa kutoka eneo ambalo Kennedy alipogwa risasi siku ya tukio la kuawa kwa Kennedy.
Katika mahojiano Ruby alisema alimuua Oswald kama kusafisha na kurudisha hadhi ya mji wa Dallas na kumuepusha machungu Jackie Kennedy (aliyekuwa mke wa JF Kennedy) ambayo angeyapatika wakati wa kufuatilia kesi dhidi ya Oswald.
Lakini ukiangalia kwa makini matamshi yake juu ya lengo lake la kumuua Oswald, haingii akilini kama ndilo lilikuwa lengo halisi la Ruby kumuua Oswald ila ni dhahili alifanya hivyo kuficha ukweli fulani ambao walihisi Oswald atauweka wazi kuhusiana na ni nani aliyemtuma akamuue Kennedy.
Baadae Ruby inasemekana alidainya kuwa mwendesha mashitaka wa awali ndiye aliyemwambia aseme hivyo wakati huo huo kiongozi wa genge moja la uhalifu katika jiji ka Vegas Johnny Roselli alidai kuwa Ruby alitumwa kumnyamazisha Oswald.
Mwaka 1965 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Oswald, na kuhukumiwa kwenda jela Ruby alisema kuwa matukio yote yaliyo zunguka mauaji ya Kennedy ukweli wake haujawahi kujulikana, na kamwe dunia haitopata kujua ukweli huo na uhalisia wa kwanini alimuua Oswald.
Pia aliongeza ya kwanmba watu walionufaika na mauaji ya Kennedy na wale waliomweka katika hali aliyonayo wakati huo kamwe hawawezi kujulikana kwasababu ukweli halisi kamwe hautojulikana.
Mwaka 1967 Ruby alifariki kwa kansa ya mapafu, lakini kabla ya kifo chake Ruby alidai ya kwamba alitembelewa na mtu aliyedai kuwa ni daktari akamchoma sindano aliyosema ya kuwa ni chanjo ya kuzuia mafua, lakini kumbe ilikuwa ni sindano ya kumpandikiza chembe chembe za seli za kamsa mwilini.
Kifo chake kilitokea wakati ambapo kesi yake ilikuwa imepangiwa kusikilizwa tena ikiwa imebainika kwamba awali haikuendeshwa vizuri, kabla ya kifo alimwambia daktari kwamba mauaji ya Kenndedy yalikuwa na lengo la kufanya mapinduzi, na walio suka huo mpango wote anawafahamu.
James Richard Worrell Jr:
Huyu alikuwa shahidi muhimu sana aliyeshuhudia mauji ya Kennedy aliyetoa majibu ya kushangaza kwa maswali ya kawaida aliyoulizwa kuhusiano la tukio hilo.
Mwaka 1963, Richard alikuwa kijana wa miaka 20 akiwa anasoma high school, ambapo siku alipouawa Kennedy Richard alikwepa kwenda shule akaenda kujiunga ma kundi la watu lililokuwa limejipanga barabarani kumlaki raisi wakati akipita.
Anasema wakati msafara wa raisi ukimpita aliskia miliomminne ya risasi, na anadai aliposkia mlio wa kwanza alipotazama kati floor ya 5 na ya 6 ya jengo lililokuwa pembeni, aliona mwanga wa bunduki utokanao na mlipuko wa risasi katika moja wapo ya dirisha la jengo hilo.
Anadai alihamaki na kuanza kukimbia na alipotulia kuvuta pumzi akaangalia kwenye mlango wa jengo hilo alimuona mwanaume akitoka nje ya jengo hilo ambapo kwa maelezo yake ya sura na umbo polisi walimfananisha na Oswald.
Miaka mitatu baadae baada ushahidi wake akiwa na rafiki yake wakiwa kwenye pikipiki, Richard alishindwa kuiongoza pikipiki jambo lilipelekea wakapata ajali na kuanguka chini ambapo kichwa cha Richard kilikanyagwa na gari, wote wawili walifariki wakiwa hoitali.
Itaendelea …..