UDSM Alumni
JF-Expert Member
- Jan 25, 2015
- 2,530
- 1,370
Bado ningependa kujua kama kuna nchi yeyote inayomiliki ziwa ama mto kwa asilimia 100 kama sehemu ya mpaka wake. Kwa hii scenario Tanzania iko sawa kuchora mpaka wake kama tunavyotambua sasa.Mpaka uliwekwa na wakoloni, na ndio mipaka hiyo hiyo tumeirithi karibu sehemu zote hapa Afrika.
Kabla ya mkoloni hakukuwa na nchi ya Tanganyika.
Tufanye kama Ukraine na dubuUnajua kwamba OAU walikubaliana kuwa mipaka ya kikoloni ndio iendelee kutumika baada ya uhuru?
Yani unataka kusema kwamba nchi za Afrika tuna busara sana kwahiyo tuanze kuchora upya mipaka. Unazijua akili za Mwafrika kweli mkuu?
Yani turudie kuchora, Uganda wapendekeze kupata Kagera salient, Kenya wapendekeze kupata mlima Kilimanjaro pale ambapo ramani ilipindishwa ili mlima uwe Tanzania, Zanzibar wadai pwani ya bara maana kuna Sultan aliwahi sema anaimiliki na akiwapa Wajerumani sijui, Tanzania tudai sehemu ya Masai Mara ya Kenya ili Wamasai wote wawe Tanzania, Kenya wapendekeze waongezewe sehemu ya ziwa Victoria wawe nayo nyingi maana Tanzania imechukua kipande kikubwa zaidi, Burundi nao waombe sehemu kubwa zaidi ya ziwa Tanganyika. Hapo ni sisi tu, bado sehemu nyingine za Afrika.
Kiuhalisia ukisoma Helligoland treaty na mkataba mwingine, hakuna ushahidi unaoonyesha Tanzania tunamiliki nusu ya ziwa Nyasa. Hata Wajerumani waliokuwa wanatawaka Tanganyika ramani yao inaonyesha Nyasa nzima ni ya Malawi.
Sisi Tanzania tunakuwa na claim kuwa wazungu walikubaliana kama kuna chanzo cha maji mpakani basi kigawanywe kila nchi inayopakana ipate kiasi chake. But that wasn't the case kwa ziwa Nyasa. Tukienda mahakama ya usuluhishi, zikaletwa mikataba na mashahidi wakoloni Tanzania tunashindwa asubuhi na mapema kabisa.
Kwa hiyo na sisi tuidai Rwanda na Burundi kuwa ni sehemu ya nchi yetu?Wamalawi si wajinga kama tunalitaka hilo Ziwa tulinunue sasa..ramani ya mjerumani ambaye ndio alionganisha makabila yote akaitengeneza Tanganyika inaonyesha ziwa Nyasa halipo kwetu, kuna agenda gani nyuma ya hili ?
View attachment 3183845
Huwa hatuzungumzi madhaifu ya ukoo mtadhaurikaAcha chuki zako za kijinga wee mwehu!! Mtu katoa maoni yake unamuhusisha na uzanzibari!! Ndio kina Lissu nyie mnaoshabikia chuki na mifarakano!??
Utoto huu.Hamna mwenye haki ya umiliki wa hilo ziwa asilimia 100.
Mipaka ya kikoloni haiwezi kutuondolea haki yetu.
Kwa hiyo maji yakizidi yakila ardhi mpaka wao nao unaongezeka?Sawa ila kunamaeneo mengine kutokana na mpaka wa ki-ardhi nadhani umefanya Tanzania kuchukua eneo kubwa kiasi kwenye maziwa
Mfano muundo wa ziwa Tanganyika na nchi zilizoizunga hilo ziwa kutokana namipaka mama ya kiardhi imefanya Zambia na Burundi kupata asilimia ndogo pia Kwa Kenya mpaka wa ardhi umenyima umiliki wakupata asilimia kubwa na hivyo hivyo Tanzania pia ingepata asilimia ndogo kwenye ziwa Nyasa kutokana na mpaka wa ardhi.
Ila tukisema tubaki hivi hivi kuwa mpaka wa ziwa Nyasa huishie pwani ya Tanzania lakini tulitumie ziwa hilo pasipo kutanabaisha mipaka hapo tunakuwa tunawasikilizia Wamalawi kuamua upepo wamatumizi ya ziwa uende vipi nahisi kama tutakuwa watumwa hivi na wanyonge kwenye maamuzi.
Mimi naona mipaka inayohusu maji tukiichukulia kuanzia kwenye mipaka ya ardhi tukafanyia makadirio ya kuiingiza kwenye ziwa au mto unagusa nchi zaidi ya moja,tunaweza tukaitatua migogoro tukandoe vinyongo.
Kwa hiyo na sisi tusitumie maji ya ziwa Victoria ambapo ndiyo asili ya mto Nile kwa kuwa mkoloni aliwekeana saini na Misri kwamba mwenye maamuzi ya mwisho wa mto Nile ni Misri?Ushahidi haupo upande wetu. Tanzania haiwezi shinda hii kesi mahakamani. Waingereza na Wajerumani wote wanajua ziwa lipo Nyasa.
Wazungu ndio waliibumba Tanganyika. Kwenye makoloni na mikataba yao ziwa Nyasa lipo Malawi.
Sasa mtu anataka Tanzania tutumie nguvu wakati suala halipo upande wetu. Last time aliyetaka kutumia nguvu kubadilisha mipaka alisababisha vita ya Kagera.
Hayo mambo ya chanzo cha maji kigawanywe katikati ni busara, ila haijaandikwa popote baina ya Malawi na Tanzania. Maandishi yaliyopo ni ya wakoloni na yanaipa Malawi ziwa lote.
Nyie na nani wakati hata Tanganyika hauijui! Wewe Tanganyika unaijua Nyerere tu! Nayo ni ya upande mmoja! Eti ilikuwa koloni la uingereza! Ingekuwa hivyo tusingekuwa hivi, tungekuwa na akili.Sisi tunachojua mpaka uko kati kati ya ziwa hizo porojo zako za Google maps wapelekee wachambawima wenzako
Nashukuru sana kwa kujenga hoja na kunipinga kwa hoja na busara kubwa, nami nitajibu hoja zako.Kama ilivyo kwa uongo; au siyo!
Mkuu 'Zanzibar ASP', niseme wazi hapa, leo unanishangaza pakubwa kweli juu ya swala hili la mpaka.
Kweli unataka sisi Tanzania tuwafundishe watoto mipaka ya nchi yao kwa kutumia taarifa za utata kama hizo za 'Google'?
Huo "ukweli' unao ung'ang'ania wewe, umeshushwa toka mbinguni, kwamba hakuna binaadam yeyote wa kuuhoji?
Kwani maswala haya ya utata wa mipaka baina ya mataifa , ni hili tu la Tanzania ndilo unalo ona wewe "ukweli" wote pasipo na shaka yoyote ; kiasi kwamba tuwaambie watoto wetu "ukweli" huo unao uona wewe?
Kama unatambua kuwa mpaka huo unalo tatizo; kwa nini ufundishe watoto bila hata ya kuzungumzia tatizo lililopo.
Wewe hujui kwamba hili swala liko kwenye usuluhishi/mazungumzo/taratibu za kulishughulikia hata kisheria..., ila unataka tu "ukweli" ufundishwe? Tanzania ikubali mipaka ya 'Google'!
Inashangaza sana.
Wabara ndio nini ?Usijali hadi zile mile kumi za sultani kutokea pwani ya kenya hadi tanganyika mnaweza kuzidai na mkazipata.
Hivi kwa nini wazanzbari mna chuki kali dhidi ya wabara
UN wanatambua Anglo-Germany treaty kama ndio msingi wa kuelezea mpaka wa Ziwa Malawi (Nyasa). Nimeona hiyo Anglo-Germany treaty, na inasema wazi Malawi ndio wamiliki wa ziwa lote la Nyasa. Tanzania tumekuwa tukiupinga huo mkataba wa Heligoland treaty kutumika kama msingi wa kujua mpaka wa Ziwa Nyasa kwa hoja kuwa haukutenda haki, una kasoro na umekosa uhalisia (jambo ambalo hata mimi naliunga mkono kwa 100%), lakini mpaka leo hii UN haijawahi kuukataa huo mkataba wa Heligoland kutumika katika kuelezea mpaka wa ziwa Nyasa. Na hukujawahi kuwepo tena mkataba mpya wa kutambua mpaka katika ziwa hilo baina ya Malawi na Tanzania.Unaweza kuwa ulipata au kuiona hata copy ya makubaliano tuliyoafikiana?
Nakumbuka yule Rais mama alitushitaki tukaitikia wito, na ikiwa kulikuwa na makubaliano ya kujadiliana nje ya mahakama huwa yanaafikiwa na pande zote mbili husika, na baada ya maamuzi upande ambao haujaridhika unaweza kukataa na kujitoa kwenye makubaliano, na kuendelea na kesi mahakamani.
Kama hatukuafikiana, bila shaka Malawi waliendelea na kesi, na labda walishinda kimya kimya, ndio maana google hufanya wafanyavyo.
Kama sio hivyo labda serikali itatujulisha watanganyika, maana hili sio la chama cha ccm bali la watanganyika wote, maana ulinzi wa mipaka yetu ni jukumu letu wananchi.
Maamuzi haya yawekwe wazi.
Sawa badi tuwape ziwa lao, haitatusaidia kuendelea kung'ang'ania mali isiyo yetu.UN wanatambua Anglo-Germany treaty kama ndio msingi wa kuelezea mpaka wa Ziwa Malawi (Nyasa). Nimeona hiyo Anglo-Germany treaty, na inasema wazi Malawi ndio wamiliki wa ziwa lote la Nyasa. Tanzania tumekuwa tukiupinga huo mkataba wa Heligoland treaty kutumika kama msingi wa kujua mpaka wa Ziwa Nyasa kwa hoja kuwa haukutenda haki, una kasoro na umekosa uhalisia (jambo ambalo hata mimi naliunga mkono kwa 100%), lakini mpaka leo hii UN haijawahi kuukataa huo mkataba wa Heligoland kutumika katika kuelezea mpaka wa ziwa Nyasa. Na hukujawahi kuwepo tena mkataba mpya wa kutambua mpaka katika ziwa hilo baina ya Malawi na Tanzania.
Mzozo uliozuka mwaka 2012 ulitokana na Malawi kutaka kuanza kuchimba mafuta katika ziwa Nyasa upande ambao Tz tunadai ni mali yetu, na Tz kutishia kuingia vitani dhidi ya Malawi, na hiyo ikapelekea Malawi kutaka kushtaki kwa kuzuiwa kutumia rasimali inazozimiliki.
Tukiweza tudai Africa nzima ni ya kwetu kwani binadamu wa kwanza aliishi Olduvai Gorge TanzaniaKwa hiyo na sisi tuidai Rwanda na Burundi kuwa ni sehemu ya nchi yetu?
Mkuu 'Zanzibar ASP', hii historia wewe ulijifunzia wapi; kwamba kuna Ziwa Malawi? Umejifunzia nchi gani historia hiyo na lini?1. Ukweli hauna mmiliki, ukweli upo siku zote na unasimama wenyewe. Ukweli ninaousema hapa, ni kile kinachotambulika kisheria kimataifa.
Ukiondoa hapa Tanzania ambapo tangu tukiwa watoto tumekuwa tukifundishwa (hewani hewani tu) kitu kinaitwa ziwa Nyasa, na ziwa hilo lipo Tanzania, hakuna mahali pengine popote duniani utakutana na hicho kitu kielimu. Dunia nzima wanajua kuna Ziwa Malawi, kiasili ni mali ya Malawi na kwa sehemu Msumbiji wamepata umiliki toka kwa Malawi.
Hivi unajua ni kwanini Tanzania haitaki kabisa watanzania walifahamu kama ni ziwa Malawi ambalo ndio jina lake rasmi kiulimwengu?
Mimi na mama yako ndio tunajua na wewe ndio hauna akili kuandika vizuri tuu hauweziNyie na nani wakati hata Tanganyika hauijui! Wewe Tanganyika unaijua Nyerere tu! Nayo ni ya upande mmoja! Eti ilikuwa koloni la uingereza! Ingekuwa hivyo tusingekuwa hivi, tungekuwa na akili.
Kuwa mzalendo; Acha ujinga. Taifa Kwanza.Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.